Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
ametangaza neema mpya kwa wafanyakazi visiwani humo baada ya
kuwakikishia kupandisha kima cha chini cha mshahara kuanzia mwaka huu
(2017).
Dkt. Shein ametoa hakikisho hilo jana
wakati akiwaongoza watanzania kuadhimisha Miaka 53 ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Amani
visiwani humo.
Alisema
kuanzia mwaka huu kima cha chini cha mshahara kitaongezeka kutoka Tsh.
150,000 hadi Tsh. 300,000 ikiwa ni ongezeko la asilimia 100.
Dkt. Shein alitoa tathmini yake ya mwaka mmoja tangu achanguliwe tena kuiongoza Zanzibar, ambapo alisema
mwaka 2016 umekuwa ni wa mafanikio makubwa katika nyanja mbalimbali
ikiwemo elimu, kilimo, viwanda, huduma za jamii ikiwemo afya na huduma
za maji, miundombinu n.k.
Akihutubia kwenye uwanja wa Amani Dkt. Shein alisema, serikali yake itaendelea kudumisha na kuenzi umoja na mshikamano ambao uliasisiwa na viongozi wa mapinduzi hayo.
Alisema,
mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kukuza pato la taifa hadi kufikia
6.6% licha ya kuongezeka kwa mfumuko wa bei kutoka 5.7% katika mwaka
2015 hadi kufikia 6.7% mwaka 2016.
Pia Dkt. Shein alieleza
utekelezaji wa sera ya kulipa pensheni kwa wazee, ambapo amesema hadi
mwezi Desemba mwaka 2016, jumla ya shilingi bilioni 4.3 zimetumika
kuwalipa wazee 25,259 waliosajiliwa kiasi cha shilingi 20,000 kila
mwezi, zoezi ambalo litaendelea kutekelezwa.
Katika hatua nyingine, Dkt Shein alitangaza
rasmi kuwa matangazo yote ya TV yatahama kutoka mfumo wa 'Analogue' na
kuhamia mfumo wa 'kidigitali' kuanzia mwezi April mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment