HATUA
ya Mahakama ya Wilaya ya Kilombero, Morogoro kumfunga Peter
Lijualikali, Mbunge wa Jimbo la Kilombero miezi sita jela, inatokana na
visa vya kisiasa
Ni
kauli ya Tundu Lissu, Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) leo mbele ya waandishi wa habari aliokutana nao kwenye Makao
Makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Lissu
ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki amesema kuwa, vita kati ya
upinzani na Chama Cha Mapinduzi (CCM) vimesababisha Lijuakali (Chadema)
kupata hukumu hiyo ya kisiasa.
Mbele ya waandishi wa habari Lissu amesema kuwa, “hiyo ni hukumu ya kisiasa” na kwamba, Jeshi la Polisi nalo limeingizwa kwenye vita hivyo.
Lissu
amesema, chanzo cha hukumu hiyo kinatokana na mgogoro wa uongozi ndani
ya Halmashauri ya Kiliombero ambapo Chadema na washirika wake wa vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) walishinda madiwani
wengi.
Hivyo, kwa mujibu wa Lissu, Halmashauri ya Kilombero ilipaswa kuongozwa na mwenyekiti anayetoka na Ukawa na awe Chadema.
“Ili
hilo lisiwezekane, na ili CCM wachukue Halmashauri ya Wilaya ya
Kilombero licha ya kushidwa kwenye udiwani, ilibidi wamfanyie
Lijualikali mambo ya ajabu,” amesema Lissu.
Lijualikali
(30) amehukumiwa jana kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki.
Huku Stephano Mgata (35), Dereva wake ambaye ni mshtakiwa wa pili
katika kesi hiyo akifungwa kifungo cha miezi sita nje.
“Kifungo cha Mh. Lijualikali ni adhabu ya kisiasa. Mh Lijualikali ni mfugwa wa kisiasa. Amefugwa kwa sababu ya siasa.
“Adhabu
ya kisisa ni vita ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi ya Chadema na
wanatumia Jeshi la Polisi, wanatumia mahakama na kwingineko. Vita hii
hii wanawatumia akina Lipumba (Profesa Ibrahim Lipumba,” amesema Lissu na kuongeza;
“Kwingine
wamemweka Lema (Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini) mahabusu kwa
miezi mitatu. Hakuna jinai yoyote. Tuliwashinda kwenye uchaguzi.
“Sasa
baada ya uchaguzi walimfungulia Lijualikali kesi ya kupinga matokeo
mahakama kuu, tukawapiga chini. Wamefungua rufaa na tunawatandika.”
Mwanasheria
huyo amesema kuwa, nchi hii ina wafungwa wa kisiasa na kwamba, pamoja
na CCM kudhani kwamba, kumfungulia kesi Lijuakali kutawapa afueni.
Wasahau.
“Tuna
wafungwa wa kisiasa nchi hii. Wale wanaofikiria kwamba kumfunga
Lijualikali CCM itapendwa na wananchi wa kilombelo wasahau hilo.
“Huwezi kuwatesa wananchi, ukatesa viongozi waliowachagua kwa mapenzi yao halafu ukategemea wakupende. Wasahau,” amesema Lissu.
Aidha,
Lissu ametoa ufafanuzi kuwa Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania inamlinda Lijualikali hivyo hawezi kupoteza ubunge
wake kutokana na hukumu hiyo.
Amesema
Chadema hakijaridhika na hukumu hiyo, hivyo kwa sasa wanaandaa
utaratibu wa kisheria ili kukata rufaa kuipinga ambapo hatua hiyo
inaweza kuchukua siku mbili kukamilika.
Timothy
Lyon, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo alisema, amemhukumu Lijualikali
baada ya kumtia hatiani kwa kosa yeye na dereva wake na kwa kuwa, mbunge
huyo alipatikana na hatia katika kesi tatu huko nyuma na kuhukumiwa
kulipa faini hivyo alistahili kutumikia adhabu hiyo.
Kesi zilkizotajwa na Lyon zinazomuhusu Lijualikali ni namba 338, namba 220 na namba 340 zote za mwaka 2014.
Katika
kesi hiyo, Dotto Ngimbwa, Inspekta wa Polisi aliiambia mahakama kuwa,
Lijuakali akiwa mshtakiwa namba moja pamoja na Mgata walitenda kosa hilo
Machi Mosi mwaka 2016 eneo la Kibaoni katika ukumbi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Kialombero na kwamba, walifanya fujo kinyume cha sheria.
Alisema
tukio hilo lilitokea Machi Mosi mwaka huo saa 4 asubuhi ambapo
washtakiwa walikana mashtaka lakini upande wa mashtaka ukathibitisha
bila kuacha shaka kwamba, walitenda kosa.
0 comments:
Post a Comment