Jeshi
la Senegal limesema kuwa majeshi ya Afrika Magharibi yataingilia suala
la Gambia usiku wa kuamkia tarehe ya mwisho wa madaraka ya Rais Yayha
Jammeh ambayo ni leo ili akabidhi madaraka kwa mshindi wa uchaguzi mkuu
uliofanywa mwezi uliopita.
Vikosi kutoka Senegal vimesogea katika mipaka ya Gambia, Nigeria pia imetuma vikosi vya anga katika eneo hilo.
Rais
wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz yuko nchini Gambia kwa kile
kilichotajwa kuwa ni juhudi za mwisho za kumshauri bwana Jammeh kuachia
madaraka kwa Rais mteule wa Gambia Adama Barrow ambaye kwa sasa yuko
nchini Senegal.
Senegali
imeomba Jumuiya ya Usalama ya Umoja wa Mataifa kushinikiza Umoja wa
nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) kuchukua hatua za msingi katika
kuhakikisha Rais mteule wa Gambia anakabidhiwa madaraka.
Chanzo: BBC
0 comments:
Post a Comment