Bado kuna utata mkubwa juu ya chanzo cha kifo cha marehemu kutokana
na kuwa na taarifa tofauti zinazokinzana. Taarifa kutoka kwa watu wa
karibu yake zinasema marehemu alikuwa anaumwa kwa takribani wiki mbili
zilizopita na alikuwa haonekani darasani wakati wakala wa marehemu huyo
(Global Education Link) ametoa taarifa na kusema kifo ni cha ghafla.
Bado uchunguzi wa chanzo chakifo hicho unaendelea. Taratibu
zakusafirisha mwili wa marehemu zinafanyika.
Chuo alichokuwa akisoma marehemu
KUHUSU KUSAFIRISHA MWILI
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa TASAFIC (Umoja wa wanafunzi
wanaosoma China) ni kwamba, gharama za kusafirisha mwili ni Dola 10000
ambayo ni sawa na 63,000RNM yaani takribani Tsh Millioni 20. Gharama
hizi zinatakiwa kulipwa na familia ya marehemu na siyo wakala wake
“Agent” japo wakala amesema atalipa halafu familia itazirudusha.
0 comments:
Post a Comment