Tume
ya Ushirikiano wa Pamoja ya Kudumu (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi,
inatarajia kukutana nchini humo kwa ajili ya kujadili masuala
mbalimbali, ikiwemo la Watanzania nane kukamatwa nchini humo kwa tuhuma
za kuingia eneo la migodini bila kuwa na kibali.
Mbali
na kujadili suala la Watanzania hao, lakini pia tume hiyo itajidili
mgogoro wa mpaka uliopo baina ya nchi hizo mbili katika Ziwa Nyasa.
Mkutano huo unatarajiwa kuanza Februari 3 hadi 5 mwaka huu nchini Malawi.
Akizungumza
Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga alisema
tume hiyo ilikuwa haijakutana kwa muda mrefu, jambo ambalo limesababisha
watu kuwa na sintofahamu kati ya ushirikiano wa nchi hizo mbili.
Kasiga
alisema mkutano wa tume hiyo, mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2003
jijini Dar es Salaam, hivyo kuwa kimya kwa muda mrefu kuna baadhi ya
watu walidhani kuwa ushirikiano wa nchi hizo mbili si mzuri.
“Kikao
kama hiki kilikaa miaka mingi kidogo… kuna masuala yaliyochelewa
kutekelezwa kutokana na kukaa kwa kikao hiki, lakini kwa sasa
yatatekelezwa kupitia vikao hivyo,” alisema Kasiga.
Aliongeza
kuwa kwa mara ya kwanza, vikao hivyo vitashirikisha wafanyabiashara
kutoka mikoa ya Njombe na Ruvuma, pia wavuvi kutoka katika mikoa hiyo
ambao wataeleza namna wanavyofanya shughuli zao kwa kushirikiana na
wenzao wa Malawi bila kuingilia.
Mindi
alisema katika kikao hicho, ujumbe wa Tanzania utaongozwa na Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk Augustine
Mahiga; na mbali na kujadili mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa na
Watanzania waliokamatwa, pia utajadili masuala mbalimbali katika sekta
za biashara, elimu, kilimo pamoja na sekta zingine.
Kasiga
pia alikabidhi tuzo za Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya
Hifadhi ya Jamii (SSRA) pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
walizoshinda kutoka Umoja wa Afrika (AU). SSRA ambayo imekuwa wa kwanza
katika Tuzo za Ubunifu Katika Sekta za Umma Afrika (AAPSIA),
ilikabidhiwa kikombe pamoja na cheti cha ushindi.
Ushindi huo wameupata kupitia mradi wao wa Mradi wa Kanzidata ya Taifa ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii.
Bi
Mindi akimkabidhi Bi. Sarah kombe la ushindi kwa niaba ya Wizara. Bi.
Kibonde aliipokea zawadi hiyo kwa niaba ya Mamlaka ya Usimamizi wa
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Meneja wa Mradi wa Mfumo wa Forodha wa TANCIS kutoka TRA akipokea zawadi ya cheti cha ushindi kutoka kwa Bi. Mindi Kasiga.
0 comments:
Post a Comment