Tuesday, 24 January 2017

KAULI YA MTATAIRO BAADA YA UPINZANI KUANGUKIA PUA UCHAGUZI MDOGO WA MARUDIO

...
Na. Julius S. Mtatiro
Goodmorning. Katika uchaguzi huu mdogo CUF ilikuwa inatetea kata 1 ya Kimwani Muleba na CHADEMA ilikuwa inatetea kata 1 ya Duru, Babati. Kata zingine zote zilikuwa za CCM na zilikuwa zinatetewa na CCM.
 
Matokeo yanaonesha CCM imetetea viti vyake vyote vya udiwani (takribani 20), CUF imenyang’anywa kiti chake kimoja (Kimwani) na CHADEMA imelinda kiti chake kimoja (Duru).
 
Kwa vyovyote vile vyama mbadala haviwezi kujivunia matokeo haya kwani havikuweza kuishinda CCM, na CCM haina cha kutambia kwani imeongeza kata moja tu. Kwa sasa nina mambo kadha ya kuzungumza;
  1. Hali halisi inaonesha kuwa kama vyama mbadala vingeshirikiana vingelishinda kata si zaidi ya 7 hivi. Bahati mbaya mashirikiano haya yalikosekana tangu mwanzo baada ya upande wa “CUF ya Msajili na Bwana Yule” kusisitiza kuwa wataweka wagombea nchi nzima na hakuna UKAWA.
  2. Lakini pia, hata shajihisho la ushirikiano mkubwa zaidi lililokuja kuzuliwa na kaka yangu Prof. Kitila Mkumbo lilifanywa TOO LATE kwa lengo la kutafuta sababu ya kujificha baada ya matokeo. Niliwahi kusema, kiuzoefu vyama haviwezi kuachiana maeneo wiki moja kabla ya siku ya uchaguzi na kushauri hivyo si kwa nia njema.
  3. Baada ya CUF ya Msajili na Bwana Yule kujipanga kuvuruga uchaguzi huu na kushusha spirit ya UKAWA, vyama vya NCCR na CHADEMA pia vilionelea kila kimoja kijipiganie jambo ambalo ni kosa kubwa. Na madhara ya migawanyiko yote yalijulikana.
  4. Uzoefu unaonesha kuwa, kuishinda CCM kwenye chaguzi ndogo ni nadra mno. Kuliwahi kuwa na mfululizo wa chaguzi ndogo, Tarime, Busanda, Tunduru, Mbeya Vijijini n.k. na kote huko CCM ilishinda isipokuwa Tarime na baadaye Arumeru. Katika chaguzi ndogo CCM hutawanya rasilimali zake nyingi zikajaa kwenye majimbo au kata hadi POMONI.
  5. Mkakati wa DOLA na CCM kuvitumia baadhi ya vyama au baadhi ya viongozi kwenye vyama (mamluki) unaelekea kufanikiwa sana. Lakini, sera za “Self Protectionism” ndani ya vyama mbadala hata kwenye mambo yanayohitaji ushirikiano wa kitaifa zitaendelea kuvigharimu vyama vyetu.
  6. Good News kwa ACT Wazalendo kwamba huenda ndicho chama kilichofanikiwa kwenye uchaguzi huu kuliko vyama vyote (CCM inclusive) kwani pamoja na uchanga wake kimevishinda baadhi ya vyama vikongwe kwenye kata chache (kwa idadi ya kura na si ushindi wa jumla). Na hiyo ni alert call kwamba ACT is needed in the UKAWA basket na kwa hiyo ianze ku BEHAVE like a true party wakati UKAWA pia ikiiandalia mazingira kisaikolojia.
  7. Bado CCM inashinda chaguzi kwa kutumia mifumo ilele; rushwa, mabavu, hila, wawakilishi wa NEC na NEC yenyewe, uwezo wa uelewa wa wapiga kura (Mfano. CCM imepeleka uandikishaji wa Bima ya Afya kwa wananchi kata ya Nkome, wakati wa uchaguzi = Rushwa).
  8. Vyama vya upinzani vinashindwa chaguzi hizi kwa sababu ya kukosa ushirikiano wa kweli baina ya vyama hivyo, maelezo namba 7 hapo juu na sentensi ya kwanza ya maelezo yaliyo namba 5 hapo juu.
  1. Kwa hakika, matokeo haya hayana athari zozote za kufaulu kwa Magufuli katika sera zake au kushindwa kwa Magufuli katika sera zake. Yaani, CCM ya Magufuli haijawa na ushawishi wa ziada kwa wapiga kura ili kupata ushindi huu kwenye ngome zake. CCM bado inashinda chaguzi kibabe na kwa mkakati dola zaidi bila kujali nani yuko madarakani.
  2. Sijaona connection yoyote kati ya matokeo haya na siasa za 2020. Vyama vyote vinayo fursa ya kuendelea kujipanga na kama tutafanikiwa kuuvunja mfumo dola unaoathiri vyombo vya uchaguzi na uhuru wake, unaoondoa mazingira sawa kwa vyama kufanya siasa n.k, mabadiliko ya kikatiba kwenye NEC na sheria za uchaguzi na mengine mengi, siasa za 2020 zitakuwa mbichi sana.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger