Mhadhiri
Msaidizi wa Chuo cha Taifa cha Usifirishaji (NIT) amekamatwa na Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Konondoni baada ya kunaswa
katika mtego wa rushwa ya ngono.
Mhadhiri
huyo anayefahamika kwa jina la Samson Jovin Mahimbo (66) mkazi wa
Makongo Juu, Dar es Salaam alikamatwa Januari 12, 2017 katika nyumba ya
kulala wageni ijulikanayo kama Camp David iliyopo eneo la Mlalakua,
Mwenge jijini Dar es Salaam.
Samson
Mahimbo alikamatwa baada ya kuwekewa mtego kufuatia taarifa iliyotolewa
na mwanafunzi huyo aliyeombwa rushwa ili aweze kumpatia alama (marks)
nzuri katika mtihani wake wa marudio (supplementary examination)
alioufanya tarehe 5 Januari 2017.
Mtuhumiwa
huyo amekamatwa kwa tuhuma za kufanya kosa hilo kinyume na kifungu cha
25 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2017.
0 comments:
Post a Comment