Aliyekuwa
mkuu wa wilaya ya Uyui Bw.Gabriel Mnyele akizungumza na Mwandishi wa
habari wa Azam tv Juma Kapipi wakati akiwa ofisi za CCM Wilaya ya Uyui
ikielezwa kuwa alikuwa ameitwa na Uongozi wa chama hicho kufuatia kuwepo
kwa taarifa kwamba ameamua kuachia ngazi nafasi ya Ukuu wa wilaya hiyo
ya Uyui jambo ambalo alilithibitisha kwa Katibu wa CCM wilaya ya Uyui
kwamba ni kweli amemwandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli.
*****
Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Gabriel Simon Mnyele amejiuzulu nafasi hiyo leo Alhamisi Januari 26, 2017 na kuwaaga madiwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano alioufanya wilayani humo.

Akieleza
sababu ya kufanya uamuzi huo, Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa
alimwandikia Rais Dkt Magufuli barua ya kujiuzulu nafasi hiyo akielezea
kusongwa na majukumu binafsi.
Bw.Gabriel Mnyele hakuwa tayari kuelezea maamuzi aliyochukua na kuwataka Waandishi waliokuwa wakihoji hatua ya maamuzi yake wasubiri tamko kutoka juu."Mimi sina la kusema kuhusu hilo nimeamua mwenyewe,kwani mmesikia kuwa nimetumbuliwa?Aliwahoji waandishi.
0 comments:
Post a Comment