Rais
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepiga marufuku viongozi wa
serikali wenye tabia ya kuwapangia bei ya mazao wakulima na kuwataka
wawaache wakulima wauze mazao yao kwa bei itakayowanufaisha wakulima
kutokana na mazao yao
Ameonya
juu ya tabia hali ilivyo sasa ambapo mkulima amekuwa akipunjwa kutokana
na bei ndogo anayolipwa pindi anapouza mazao yake.
Rais
Magufuli ametoa agizo hilo leo wakati ambapo amemaliza ziara ya siku
mbili mkoani Simiyu na kuanza rasmi ziara ya siku mbili mkoani Shinyanga
na kuahidi kuendelea kuulinda Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar
kwa nguvu zake zote
Rais
Magufuli amesema Mapinduzi matukufu ya Januari 12,1964 ndio
yaliyosababisha kuwepo kwa Muungano kati ya Tanzania Bara na Zanzibar na
hivyo kuzaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo kuna umuhimu
mkubwa kwa Watanzania kuuenzi na kuulinda kwa manufaa ya wananchi wote.
''
leo ni siku muhimu sana kwetu Watanzania kwa kuwa siku hii ya Januari
12,1964 miaka 53 iliyopita ndio siku yalipofanyika Mapinduzi matukufu
ya Zanzibar yaliyopelekea kuondolewa kwa utawala dhalimu wa kikoloni na
kupelekea kuzaliwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya
Tanzania Bara na Zanzibara kuungana,hivyo tuna kila sababu ya kuienzi
siku hii muhimu'' amesema Rais Magufuli.
Akiwa
Wilayani Maswa mkoani Simiyu mara baada ya kutembelea kiwanda cha
kutengenezea chaki na kuweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa barabara ya
Mwigumbi hadi Maswa yenye urefu wa kilomita 50.3 kwa kiwango cha lami,
Rais Magufuli amewataka wananchi wa mkoa wa Simiyu kutumia barabara hiyo
kujiletea maendeleo.
Rais
Magufuli ameupongeza mkoa wa Simiyu kwa kutekeleza kwa vitendo Sera ya
Serikali ya awamu ya Tano ya Tanzania ya viwanda kwa ujenzi wa kiwanda
cha Chaki na kutoa wito kwa uongozi wa kiwanda hicho kuongeza
uzalishaji wa chaki ili ziweze kukidhi soko la nchi nzima badala ya
mikoa kumi ya sasa inayotumia chaki zinazozalishwa na kiwanda hicho.
0 comments:
Post a Comment