KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesema mgogoro wa Zanzibarna anaamkni atakuwa Rais Zanzibar.
Amesema, mgogoro visiwani humo utamalizika endapo viongozi wa vyama vyote va siasa watakaa chini kufanya mazungumzo.
Akizungumza katika mahojiano katika kipindi cha Funguka kinachorushwa
na Kituo cha Televisheni cha Azam, Maalim Seif alisema jambo la muhimu
ni viongozi kukubali Zanzibar kuna tatizo.
Alisema anaamini kama kuna nia njema, maridhiano yanaweza kupatikana Zanzibar na migogoro yote ya kisiasa kumalizika.
“Hii naamini kabisa, kama kuna nia njema, kila upande ukubali
Zanzibar kuna tatizo, ukubali kuna haja ya viongozi kupata ufumbuzi wa
tatizo na watapata vipi, ni kwa kushirikiana pamoja,” alisema Maalim
Seif aliyewahi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais katika Serikali ya Umoja wa
Kitaifa Zanzibar.
Alisema Serikali iliyopita ya Umoja wa Kitaifa, ilikuwa na mafanikio
makubwa na kwamba anavyoona hakuna kitakachorudisha hali ile, kama si
kwa vyama kushirikiana.
“Kila upande ukiona unawakilishwa itasaidia kuleta Wazanzibari pamoja,” aliongeza Maalim Seif.
Aidha, Maalim Seif alisema anajua kuna majaribio makubwa yanafanywa
kutafuta ufumbuzi, hivyo ufumbuzi ni vema upatikane ili kuridhisha pande
zote, na kwamba kuna njia nyingi ya kupata muafaka na hiyo ni pamoja na
kufanyika mazungumzo, lakini ni baada ya kila upande kukubali kuwa
Zanzibar kuna tatizo.
Akizungumzia kugombea tena nafasi ya urais mwaka 2020, Maalim Seif
alisema ni vema kusubiri ili kuona hali ya kisiasa itakapofika wakati
huo.
“Tusubiri kwanza wakati wake tuone kama tunafanikiwa au hatufanikiwi
kwenye hili, halafu tutafanya maamuzi,” alisema Maalim Seif ingawa
baadaye alisema kuwa karibuni anatarajia atakuwa Rais wa Zanzibar.
“Natarajia muda mfupi ujao, Inshaallah nitakuwa Rais wa Zanzibar,”
alisema bila kufafanua anawezaje kuwa rais wakati hakushiriki uchaguzi
mkuu wa Machi, 2016.
Akizungumzia mgogoro ndani ya CUF, Hamad alisema Msajili wa Vyama vya
Siasa aliruhusu upande wa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim
Lipumba kuchukua Sh milioni 369 ambazo ni fedha za ruzuku na kwamba
baadaye chama kitashindwa kuzijibia matumizi yake.
Kuhusu hilo, alisema wamemwandikia Msajili, Gavana wa Benki Kuu (BoT)
na pia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), waangalie
hatua ya kuchukua.
Akizungumzia afya yake, alisema anamshukuru Mungu kwamba afya yake ni
njema. Hata hivyo alisema tangu aondoke madarakani, amekuwa
akijihudumia mwenyewe katika matibabu na si fedha za serikali ikiwa ni
pamoja na matibabu nchini India.
0 comments:
Post a Comment