Mkazi
wa Temeke Mikoroshoni, Miradji Sanyero, jana alipatwa na mkasa wa
kutumbukia katika ‘chemba’ ya kupitishia maji taka yenye urefu zaidi ya
futi 12, iliyopo eneo la Bakhresa, Tazara, Barabara ya Mandela jijini
Dar es Salaam.
Alipatwa na mkasa huo akiwa katika harakati ya kujitafutia maisha,
ambapo ghafla alitumbukia katika chemba hiyo iliyokaa vibaya katika
mlango mkuu unaotumiwa na magari makubwa wa ofisi za Bakhresa.
Akijojiwa, akiwa mahututi, alisema “Nilikuwa napita jirani huku
nikichukua tahadhari nisigongwe na magari yanayoingia na kutoka katika
ofisi hizo, ndipo nikajikuta ghafla nimetumbukia ndani ya chemba hii na
kuumia kidole cha mkono wa kulia, miguuni na mbavu ambazo sasa zinauma
sasa”.
Wafanyabiashara wadogo (machinga) wa eneo hilo, walisema chemba hiyo ni
hatari na watu kadhaa wametumbukia katika kipindi cha hivi karibuni.
Walidai huyo alikuwa mtu wa tatu.
“Tunaomba Tanroads wafike eneo hili, waone kisha wazibe chemba hii. Kama
hawatafanya hivyo, kuna hatari ya kupoteza maisha hasa watoto wadogo
ambao uwezo wao wa kuhimili vishindo ni mdogo sana” alisema machinga
mmoja, Ali Tematema.
Gazeti hili lilishuhudia baadaye trafiki wakishirikiana na wananchi,
wakimsaidia Sanyero kwenda kupanda bajaji kwenda Polisi kuchukua Fomu
Namba 3 ili aende hospitali kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.
Chanzo-Habarileo
0 comments:
Post a Comment