Shuti
la ‘mwendokasi’ la umbali usiopungua mita 25 la kiungo Himid Mao
limetosha kuamua matokeo ya mchezo wa Fainali ya Mapinduzi uliofanyika
mjni Zanzibar.
Miamba hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliichapa Simba bao 1-0 na kutosha kutangazwa mabingwa wapya wa Kombe la Mapinduzi.
Wakinolewa
na kocha wa vijana wa Azam, Idd Cheche aliyechukua kwa muda mikoba ya
Zeben Hernandez aliyetimuliwa kwa matokeo mabaya, Azam FC iliibuka na
ushindi wa bao la dakika ya 13 lililofungwa na kiungo huyo wa Taifa
Stars, Himid.
Ushindi huo pia umeifanya Azam FC kutwaa taji la tatu la Kombe la Mapinduzi baada ya awali kulitwaa miaka ya 2011 na 2012.
Katika
mashindano hayo, beki wa Simba, Method Mwanjali amechaguliwa kuwa
mchezaji bora wa Mapinduzi Cup, tuzo ya kipa bora imekwenda kwa Aishi
Manula wa Azam FC, timu bora ya vijana ni Taifa Jang’ombe.
Mfungaji
bora ni kiungo wa Yanga, Saimon Msuva, aliyeweka kimiani mabao manne,
wakati mwamuzi bora wa mashindano hayo akichaguliwa kuwa Mfaume Ali.
0 comments:
Post a Comment