Sunday, 15 January 2017

AJIRA KWA WALISOMA CHUO CHA MAJI, SERIKALI YAONESHA DALILI

...
IMG_1377
Uongozi na wanafunzi wanaosoma kwenye Chuo cha Maji, wameiomba serikali kusaidia kuwa na mpango bora wa upatikanaji wa ajira kwenye halmashauri na mamlaka za miji kwa wahitimu wa chuo hicho, ambacho kimekuwa wakala wa serikali tangu mwaka 2008.
Chuo cha Maji ambacho ni chuo pekee kikiwa na jukumu la kutoa mafunzo katika kiwango chenye ubora kwa ajili ya kupata mafundi sanifu wa maji nchini pamoja na ushuri wa kitaalam kwenye sekta ya maji, kinakabiliwa na changamoto ya wahitimu wake kukosa ajira kwa kiwango kikubwa hivyo kushindwa kutimiza malengo yake tangu kuanzishwa kwake mwaka 1974.
Kwa sasa wahitimu wengi wanaopitia kwenye chuo cha Maji kilichopo jijini Dar es salaam wanakabiliwa na ukosefu wa ajira licha ya uhaba mkubwa uliopo nchini wa wataalamu wa sekta ya maji kwa ngazi za stashahada kwenye halmashauri na mamlaka mbalimbali za miji hapa nchini.
Hayo yamebainishwa na uongozi wa Chuo cha Maji pamoja na wahitimu 313 wa stashahada mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho wakati wa mahafali ya nane yaliyofanyika jijini Dar es salaam, ambapo serikali iliwakilishwa na naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi  ISACK KAMWELWE.
Kwa upande wake Serikali imewataka wahitimu wanaomaliza kwenye chuo hicho kuwa licha ya kwamba inakusudia kutangaza nafasi za mafundi sanifu wa maji nchi nzima lakini pia wawe na ujasiri wa kujiajiri kwa kujiunga pamoja katika vikundi na kutumia ujuzi wao waliopata chuoni.
Katika mahafali ya nane ya Chuo cha Maji, jumla ya wahitimu 313 walitunukiwa stashahada za uhandisi wa usambazaji maji na usafi wa mazingira, Hadrojiolojia na Uchimbaji wa Visima, Haidrolojia na hali ya Hewa, Teknolojia  ya maabara ya Ubora wa Maji na Uhandisi wa Umwagiliaji.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger