Image captionUrusi inalalamikiwa kudukua taarifa za uchaguzi wa Marekani 2016
Mkurugenzi
wa usalama wa Marekani James Clapper, kitendo cha Urusi kuingilia
uchaguzi wa Marekani mwaka uliopita kilikuwa cha ajabu kushuhudia katika
utendaji kazi wake.
Akizungumza
katika Baraza la senate Nchini Marekani, Clapper amesema udukuzi huo wa
barua pepe za chama cha Democratic kuelekea uchaguzi uliofanyika mwezi
Novemba ulisimamiwa na Raisi wa Urusi Vladimir Putin, na kuongeza kuwa
atatoa taarifa kamili kwa umma wiki ijayo.
Mkurugenzi wa usalama wa Marekani James Clapper
Clapper
amesema kuwa ifikapo ijumaa atatoa mchanganuo wa tafiti zake kwa Rais
mteule wa Marekani Donald Trump aliyewahi kulaani na kutilia shaka
ushiriki wa Moscow.
Urusi pia imekanusha madai ya kuhusika katika udukuzi huo.BBC
0 comments:
Post a Comment