Hilo ni ongezeko la ajali 2,009 ambazo ni sawa na asilimia 36.5. Aidha kuna ongezeko la vifo 9 ambapo kwa kipindi kama hicho mwaka 2015 vilitokea vifo 316 ikilinganishwa na vifo 325 vilivyotokea mwaka jana ambavyo ni sawa na ongezeko la asilimia 2.7.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama barabarani kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Desemba 2016, ikilinganishwa na Januari hadi Desemba mwaka 2015.
“Pia kuna ongezeko la watu 654 waliojeruhiwa kwani Januari hadi Desembwa mwaka 2016 walijeruhiwa watu 4,066 ukilinganisha na watu 3,412 waliojeruhiwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2015 sawa na asilimia 16” alisema.
Alisema kwa upande wa makosa yaliyokamatwa, kuna ongezeko la makosa 382,207 kwani katika kipindi kama hicho mwaka jana yalikamatwa makosa 769,170 yaliyoiingizia serikali maduhuli ya Sh 23,065,020,000 ikilinganishwa na makosa 386,963 yaliyoiingizia serikali maduhuli ya Sh 11,608,700,000 kwa mwaka 2015, ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 49.6.
Takwimu za ajali za pikipiki, zimeonesha kuna upungufu wa ajali 168. Kwa kipindi kama hicho mwaka jana zilitokea ajali za pikipiki1036 ikilinganishwa na ajali 1,204 zilizotokea mwaka 2015 ambazo ni sawa na asilimia 13.9.
Sirro alisema kwa upande wa vifo vilivyotokana na ajali za pikipiki vimepungua kwa idadi ya watu nane kwani Januari hadi Desemba mwaka jana watu 80 walifariki kutokana na ajali za pikipiki ikilinganishwa na watu 88 waliofariki mwaka 2015 sawa na upungufu wa asilimia tisa.
Pia alisema majeruhi wa ajali za pikipiki nao wamepungua watu 225 kwani Januari hadi Desemba 2016 walijeruhi watu 904 ikilinganishwa na watu 1,129 waliojeruhiwa mwaka 2015 ambao ni sawa na asilimia 20.
0 comments:
Post a Comment