Siku moja baada ya Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako kusema waandishi waliomuandika vibaya watakufa kabla ya Machi 2017, Jeshi la Polisi linatarajia kutoa msimamo wake dhidi ya kauli hiyo leo.
Kauli hiyo ya Mzee wa Upako aliyoitoa juzi kanisani kwake, ilikuwa
ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo
akijibu yale yaliyoandikwa katika vyombo vya habari kuhusu madai ya
kulewa na kumfanyia fujo jirani.
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro jana
alisema ni mapema kuzungumzia sakata hilo kwa sababu jana ilikuwa
sikukuu na atatolea ufafanuzi leo.
“Anasema hao waandishi watakufa kabla
ya Machi 2017 kwani yeye Mungu? Hilo ni suala zito, tumeandaa mkutano
na waandishi wa habari tutalizungumzia suala hilo kesho (leo),” alisema
Kamanda Sirro.
Katika kauli hiyo, Mzee wa Upako alisema kila mwandishi
aliyemuandika vibaya ikifika Machi mwakani hatakuwa hai na kama
wataendelea kuishi, ataacha kazi ya kuhubiri injili na kwenda kuuza
gongo.
0 comments:
Post a Comment