MAKUBWA!
Mwanadada mkongwe wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C,’ amedaiwa
kuwageuza mtaji wanaume wanaojitokeza kumchumbia kwa kuwapiga mizinga
ili ajipatie ‘chochote’ (fedha), Risasi Mchanganyiko lina ‘full’ stori.
Kwa mujibu wa mmoja wa wanaume
aliyejitambulisha kwa jina la Aboubakar ambaye alifunga safari mpaka kwa
Ray C kwa lengo la kutaka kumuoa wiki chache baada ya mwanadada huyo
kutangaza kutafuta mume mwenye vigezo alivyovitaka, baada ya kuchati na
kumueleza kuwa anataka kumuoa, alishangaa kuona mwanadada huyo anampiga
mzinga.
Kijana Abubakar Ally ‘Babuu’.
Aboubakar alisema Ray C alimuomba
amtumie shilingi laki moja kwa njia ya simu ambapo jamaa huyo alikataa
na kutaka wakutane kwanza ndiyo wapeane kiasi hicho cha fedha. Msanii
huyo alimtaka jamaa wakutane Mbezi-Garden lakini amtumie kwanza pesa
hizo.
Akizidi kumwaga ubuyu, Aboubakar alisema
alianza kumuona Ray C kama mtu wa mizinga kwa kung’ang’ania atumiwe
pesa hiyo wakati hawajakutana na kuongeza kuwa alimpigia simu ili kupata
uhakika zaidi kama kweli akimtumia pesa hiyo watakutana kwenye hoteli
hiyo, lakini alimhakikisha kuwa endapo atamtumia watakutana.
“Unajua nini, ningeweza kumtumia kama
tungekutana ana kwa ana lakini ndiyo kwanza nimewasiliana naye ananipiga
kirungu kikubwa hivyo je, nikiwa naye si nitakuwa natoa mamilioni, kama
ndiyo hivyo amenishinda,” alisema Aboubakar.
….Akigonga geti nyumbani kwa Ray C.
…Kama hiyo haitoshi, mwanaume mwingine
kutoka Mwanza aliyeongea na mwandishi wetu kwa sharti la kutoandikwa
jina lake gazetini, alidai kuwa Ray C alimwambia amtumie shilingi elfu
40 kwa ajili ya mafuta kwenye gari lake kabla hata hajakutana naye jambo
lililomfanya aachane naye.
“Aliniambia nimtumie shilingi elfu 40,
sasa nikaona mtu mwenyewe ndiyo kwanza ninaongea naye, anaonekana
anapenda hela sana huyu mdada na mimi nimekata tamaa,” alisema mwanaume
huyo.
Mwandishi wetu alimtafuta Ray C na
kumsomea mashtaka yake ambapo alisema wanaume wengi wamekuwa wakimsumbua
baada ya kutangaza kutaka mume na kudai kuwa wanaume hao ni washamba
hivyo ameamua awaombe hela ili wasimpigie tena.
“Wapuuzi sana hao, sasa kuwakatiza
nawaambia tuma milioni baada ya hapo hawanisumbui tena,” alisema Ray C
na alipoulizwa kama haoni anajikosesha bahati ya mume mwema kwa kuwaomba
hela, alisema wanaume wengi wanaopiga ni washamba tu kwa kuwa yeye
hataki kulea mwanaume bali anataka kulelewa
0 comments:
Post a Comment