Saif al-Islam Gaddafi.
SAIF al-Islam Gaddafi ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Rais wa Libya,
Muammar Gaddafi, amehukumiwa kunyongwa katika mahakama moja nchini Libya
pamoja na watu wengine nane kufuatia uhalifu wa kivita uliohusishwa na
mapinduzi ya mwaka 2011.Watuhumiwa hao walikuwa wameshtakiwa pamoja na washirika wengine wa kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani kwa kujaribu kuzima maandamano wakati wa mapinduzi hayo.
Saif al Islam, ambaye kwa sasa anazuiliwa na kundi moja la waasi la zamani katika Mji wa Zintan hakuwepo mahakamani na alitoa ushahidi wake kupitia teknolojia ya kanda ya video.
0 comments:
Post a Comment