
WATOTO wawili wa familia moja, Nuru (3) na Dora Kaitaba (2), wamefariki dunia kwa kuungua moto hadi kubaki majivu baada ya moto mkubwa uliotokana na petroli kulipuka nyumbani kwao, Mapinga, Bagamoyo mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa mashuhuda, baba mzazi wa watoto hao, Kaitaba ambaye ni mpiga picha wa kujitegemea, alikuwa amerejea kutoka Bunju B alikofuata petroli ambayo huiuza katika vipimo vidogo vya kwenye makopo ya maji nyumbani hapo.
Ilizidi kudaiwa kuwa alipofika kwake alishusha mzigo wa mafuta, watoto wake hao walikuwa wamelala katika kibanda chake cha biashara.
“Baada ya kuwasha mshumaa, moto huo ulidakwa na petroli hiyo iliyokuwa kwenye dumu na kusababisha mlipuko mkubwa.
Watu wakiwa wanaangalia tukio hilo kwa masikitiko makubwa, Kikosi cha Zimamoto Bagamoyo kiliwasili kikiwa kimechelewa hivyo kuambulia kuchukua majivu ya watoto hao wawili waliaochana mwaka mmoja kuzaliwa.
Aidha Kamanda Matei alitumia fursa hiyo kupiga marufuku biashara hiyo ya mafuta ya petroli na dizeli ambayo ni maarufu wilayani humo.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, Amina.
0 comments:
Post a Comment