Monday 23 June 2014

MMUME WA FLORA MBASHA:MWAKA WA MAJANGA KWANGU NIMETAPELIWA HATI YA NYUMBA NA VIWANJA

...

MAJANGA! Siku chache baada ya kuachiwa kwa dhamana katika kesi ya kudaiwa kumbaka shemejiye, mwimbaji wa Injili na mfanyabiashara Bongo, Emmanuel Mbasha amedaiwa kuibiwa hati za nyumba na viwanja.
Mfanyabiashara Bongo, Emmanuel Mbasha mume wa Flora Mbasha.
Chanzo makini kilichomo ndani ya familia, kimedai kuwa mara baada ya Mbasha kujitokeza na kuwekwa mahabusu Juni 17, mwaka huu, mtu asiyejulikana alikwenda nyumbani kwa mfanyabiashara huyo, Tabata-Kimanga, Dar na kukwapua hati za nyumba na viwanja mbalimbali anavyovimiliki.
...Siku aliyopandishwa kizimbani.
“Mbasha hakukuta kitu pale nyumbani, vilikombwa vyote sijui na nani. Inauma sana kwani mtu ndiyo kwanza ametoka mahabusu halafu anakuta nyumbani kwake hakuna vitu muhimu kama hivyo, inasikitisha sana,”  kilisema chanzo hicho.
Kikizidi kumwaga data, chanzo hicho kilisema katika vitu vilivyoibwa ni pamoja na nyaraka mbalimbali zikiwemo hati za viwanja kadhaa vilivyopo Iringa, kadi ya gari na vitu vingine vidogovidogo.
Baada ya kunyaka madai hayo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Mbasha ili kujua ukweli wa ishu hiyo ambapo alipopatikana alikiri kutovikuta vitu hivyo muhimu nyumbani kwake.
“Ni kweli kama ulivyosikia ila nisingependa kuzungumzia kila kitu kwa sasa nahitaji kupumzisha akili,” alisema Mbasha.
Mbasha aliyetoka kwa dhamana Juni 19, katika kesi hiyo ya kudaiwa kubaka iliyosomwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, kesi yake itatajwa tena Julai 17, mwaka huu.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger