Friday 27 June 2014

MAMA AMUUNGUZA MTOTO WAKE WAKUMZAA MDOMO JIJINI DAR ES SALAAM

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Asha (31) ambaye ni mke wa mtu, amejikuta akiachika katika ndoa yake baada ya kudaiwa kumuunguza midomo mwanaye, huko Yombo Buza, jijini Dar, Juni 24 mwaka huu.
Paulina, akiwa na majeraha ya moto midomoni.
 
Kwa mujibu wa majirani, mwanamke huyo alimchoma mtoto wake wa kumzaa, Paulina, mwenye umri wa miaka mitano kwa kile alichodai kuwa tabia yake ya kudokoadokoa fedha za mtaji wake wa biashara ya samaki.
Majirani hao walisema kuwa walimuona mama huyo akichochea moto wa kuni katika jiko lililokuwa nje ya nyumba yake, kabla ya kuingia ndani akiwa na fito moja inayowaka na muda mfupi baadaye wakasikia mtoto huyo akilia kwa sauti iliyoonyesha kupata maumivu makali.
Kilio hicho kiliwashtua majirani hao ambao waliamua kuingia ndani ya nyumba hiyo, lakini katika hali ya kushangaza, walimkuta mama huyo ameshikilia kuni yenye moto huku mtoto huyo akiwa na majeraha ya kuchomwa moto midomoni na mguuni.
Baada ya kuona hivyo, walimshurutisha kuacha unyama huo na badala yake ampeleke hospitali, lakini mama huyo alikataa katakata, akidai hawezi kufanya hivyo hadi binti huyo mdogo atakapoacha tabia yake.

Kuona hivyo, majirani hao walitoa taarifa Kituo cha Polisi cha Buza ambapo askari walifika eneo la tukio wakiongozana na mwanaharakati wa haki za watoto kutoka taasisi binafsi ya Tuhimizane Children Academy, Cleophas Simeone, ambao walimkamata na kumfikisha kituoni alikofunguliwa jalada lenye namba CHA/RB/5521/2014, UKATILI DHIDI YA MTOTO.
Mwanaharakati huyo aliwasiliana kwa njia ya simu na baba mzazi wa mtoto huyo aliyedai yupo nje ya Dar es Salaam kikazi ambapo baada ya kusimuliwa kilichotokea, aliagiza mwanamke huyo kuondoka nyumbani kwake muda huohuo na kumuomba Simeone aendelee kukaa na mwanaye ambaye ameshaanza matibabu, hadi atakaporejea
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger