Monday 30 June 2014

DR SALIM AFICHUA SIRI YA JT NA TUME YA WARIOBA

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
                                                      “Ni vizuri viongozi wakaandaliwa, isiwe mtu anaibuka tu anagawa hela halafu anashinda. Anatakiwa mtu atakayeweza kushughulikia matatizo ya Watanzania. Watanzania ni wapole na wavumilivu lakini wanazungumza. Hivyo anahitajika kiongozi atakayesikiliza mahitaji yao na kutoa suluhisho, si kutoa ahadi za uongo,” Dk Salim Ahmed Salim
KWA UFUPI
Abainisha ilikuwa ikimpa taarifa kwa kila hatua iliyokuwa ikifikia, asema alishangaa kumsikia akiikosoa katika Bunge la Katiba
Dk Salim: Sina mpango na urais 2015

Dk Salim apongezwa
Dar es Salaam. Waziri Mkuu Mstaafu, Dk Salim Ahmed Salim amesema hakutarajia kusikia kauli za Rais Jakaya Kikwete alizozitoa bungeni kukosoa Rasimu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa sababu walikuwa wanampa taarifa kwa kila hatua waliyokuwa wanafikia kabla ya kutoa rasimu hiyo.
Dk Salim alitoa kauli hiyo katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake Masaki, Dar es Salaam wiki iliyopita.
“Hatukutarajia kama hali ingefikia hatua iliyofikia,” alisema Dk Salim na kuongeza: “Lakini Rais ana uamuzi wake na anazingatia mambo mengine mengi.”
Akilihutubia Bunge maalumu la Katiba Machi 21, mwaka huu Rais Kikwete aligusia mambo saba ya msingi yaliyomo katika Rasimu ya Katiba na kutaka yatazamwe kwa kina, huku akibainisha kuwa mengine hayawezekani kutekelezeka. Miongoni mwa mambo hayo ni muundo wa Serikali. Alipinga waziwazi pendekezo la serikali tatu lililopendekezwa na Tume na kuegemea katika muundo wa serikali mbili na idadi ya watu walioupendekeza akionyesha kuwa ilikuwa ni ndogo.
Pia alisema ni vigumu kutenganisha uwaziri na ubunge kama ilivyokuwa imependekezwa na Tume kwa maelezo kuwa mawaziri wanatakiwa kuwepo bungeni ili kujibu hoja za Serikali.
Jambo lingine alilokosoa katika Rasimu ni pendekezo la mtu kupoteza ubunge kwa sababu ya kuugua kwa miezi sita mfululizo huku akisema baadhi ya vifungu vya Katiba vinayopendekezwa vimekuwa na mambo mengi ambayo hayapaswi kuwamo katika Katiba, bali katika sheria zinazotafsiri utekelezaji wa Katiba yenyewe.
Katika mahojiano hayo maalumu, Dk Salim alisema baada ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume aliacha kuhudhuria vikao vya chama chake ili aweze kufanya kazi hiyo kwa usahihi na alimtaarifu Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais na katibu mkuu wake na walimwelewa.
Alipoulizwa anaitazama vipi Tanzania iwapo Katiba Mpya haitapatikana, Dk Salim alisema ana wasiwasi kwa kuwa suala hilo limeingizwa siasa na Bunge Maalumu limegeuka la kisiasa hivyo linaweza kuleta matatizo.
“Tuko katika hali ambayo si nzuri inayohitaji uongozi thabiti, viongozi wote watambue umuhimu wa zoezi hili kwa lengo la kulinda amani na utulivu wa nchi yetu,” alisema.
Alisema kunahitajika ufumbuzi wa kudumu na hicho ndicho kipimo cha uongozi kwa CCM, Chadema na wengine kwa kutafakari masilahi ya Watanzania wa leo, kesho na keshokutwa.
Nini kifanyike?
Dk Salim alisema jambo muhimu sasa ni pande mbili zinazoshindana kuhusu idadi ya Serikali kutumia mwezi ujao wa Julai kukaa pamoja na kumaliza tofauti zao ili Bunge la Katiba liendelee bila misuguano.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger