
ASKARI wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kambi ya Pangawe mkoani Morogoro wamemuokota mtoto mwenye umri wa miaka sita, Mwajuma Athuman aliyedai kukimbia mateso kutoka kwa mama yake mkubwa Juni 17, mwaka huu.
Mwandishi wa habari hizi alimkuta mtoto huyo akiwa na makovu kichwani na kidonda kikubwa mguuni kilichosababisha ashindwe kutembea ambapo alidai kilitokana na kipigo kutoka kwa mama yake huyo.
“Nimekimbia nyumbani, mama ananipiga kila siku nikitoka shuleni, nilifika kambi ya jeshi kwa mtoto mwenzangu ninayesoma naye lakini nilipotea nyumba yao.
Kuhusu wazazi wake, mtoto huyo alisema mama yake alifariki dunia yeye akiwa na umri wa miaka miwili, baba yake anaishi Mwanza ambako ameoa mke mwingine. Mama mkubwa huyo huyo alipoitwa mbele ya viongozi wa serikali ya mitaa, alikiri kuishi na mtoto huyo, lakini alikanusha kumtesa.
Hata hivyo, mwanamke huyo alingíangíania kumchukua mtoto wake ili arejee naye nyumbani, lakini viongozi hao waligoma na kwa zaidi ya siku nne aliishi nyumbani kwa Mohamed Said.
0 comments:
Post a Comment