Monday 30 June 2014

MECHI KATI YA BRAZIL VS COLOMBIA: BRAZIL YAIFUNGA COLOMBIA MARA 15 KATIKA MECHI 25

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Nyota wa Brazil, Neymar akishangilia mojawapo ya mabao aliyoifungia timu yake katika fainali zinazoendelea

MECHI ya robo fainali baina ya Brazil na Colombia ni ya kwanza kabisa kwa timu hizo mbili za Amerika Kusini kupambana
kwenye mashindano ya fainali za Kombe la Dunia, lakini ni ya 26 kuzikutanisha timu hizo katika historia yao.
Ukitazama rekodi vitabuni, unaweza kusema kwamba Colombia ni vibonde wa Brazil, kwani katika mechi 25 walizocheza tangu mwaka 1945 mpaka sasa, Brazil imeshinda jumla ya 15, kutoka sare mara nane na kufungwa mechi mbili tu.
Kwa ujumla wake, Brazil imefunga mabao 55-11, ikiwa ni rekodi kubwa mno ya mabao.
Timu hizo zimepambana mara 10 katika mashindano ya awali ya Kombe la Dunia ambapo katika mechi hizo Brazil imeshinda mara tano na kutoka sare mara tano pia.
Aidha, katika mashindano ya Ubingwa wa Amerika Kusini maarufu kama Copa America (zamani yakijulikana kama South American Championship), timu hizo zimepambana mara tisa na Brazil imeshinda mara saba, kutoka sare moja na kupoteza moja.
Zilipopambana katika mashindano ya 7 ya Kombe la Dhahabu (Gold Cup) kule Miami, Marekani mwaka 2003, Brazil ilishinda kwa mabao 2-0.

Katika mechi za kirafiki, timu hizo zimepambana mara tano, na hapa pia Brazil ikashinda mara mbili, sare mbili na kupoteza mechi moja.
Kwa rekodi hizo, haijajulikana mchezo wao war obo fainali utakuwa na matokeo gani, ingawa kwa ujumla mpira unadunda na mpaka filimbi ya mwisho itakapopulizwa ndipo mwamba atakapojulikana. Na hapa ijulikane wazi kwamba hakutakuwa na sare, lazima mshindi apatikane hata kwa shilingi.
Takwimu kamili ni hizi:
Ubingwa wa Amerika Kusini
21/01/1945 Colombia 0-3 Brazil - Santiago, Chile
17/04/1949 Brazil 5-0 Colombia - São Paulo, Brazil
24/03/1957 Colombia 0-9 Brazil - Lima, Peru
14/03/1963 Brazil 5-1 Colombia - La Paz, Bolivia
07/07/1989 Brazil 0-0 Colombia – Salvador, Brazil
13/07/1991 Colombia 2-0 Brazil – Viña del Mar, Chile
19/07/1991 Brazil 2-0 Colombia – Santiago, Chile
13/07/1995 Colombia 0-3 Brazil – Rivera, Uruguay
19/06/1997 Brazil 2-0 Colombia – Santa Cruz, Bolivia
Michuano ya awali Kombe la Dunia
06/08/1969 Colombia 0-2 Brazil – Bogotá , Colombia
21/08/1969 Brazil 6-2 Colombia – Rio de Janeiro, Brazil
20/02/1977 Colombia 0-0 Brazil – Bogotá, Colombia
09/03/1977 Brazil 6-0 Colombia – Rio de Janeiro, Brazil
28/03/2000 Colombia 0-0 Brazil – Bogotá, Colombia
15/11/2000 Brazil 1-0 Colombia – São Paulo, Brazil
07/09/2003 Colombia 1-2 Brazil – Barranquilla, Colombia
13/10/2004 Brazil 0-0 Colombia – Maceio, Brazil
14/10/2007 Colombia 0-0 Brazil – Bogotá, Colombia
15/11/2008 Brazil 0-0 Colombia – Rio de Janeiro, Brazil
Gold Cup
19/07/2003 Brazil 2-0 Colombia – Miami, Marekani
Mechi za kirafiki
01/02/1981 Colombia 1-1 Brazil – Bogotá, Colombia
25/04/1985 Brazil 2-1 Colombia – Belo Horizonte, Brazil
15/05/1985 Colombia 1-0 Brazil – Bogotá, Colombia
20/12/1995 Brazil 3-1 Colombia – Manaus, Brazil
15/11/2012 Colombia 1-1 Brazil – New Jersey, Marekani
Msimamo
Brazil 25 15 8 2 55- 11 53
Colombia 25 2 8 15 11- 55 14
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger