Saturday 28 June 2014

AJALI YA NOAH SINGIDA-WATATU WAFARIKI,KUMI WAJERUHIWA

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Watu watatu wamekufa na wengine kumi wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noha kupasuka tairi ya nyuma na kubingirita mara tatu katika kijiji cha Januka manispaa ya Singida.


Akithibitisha kitokea kwa vifoo hivyo mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida daktari Deogratias Banuba amesema wamepokea maiti mbili wakiwa wamesha fariki eneo la tukio akiwemo dereva wa Noha bwana Enock Mbaga, binti Ajira Juma na maiti nyingine ya Bi Tatu Bunku ambaye alikuwa herd mistres Ngimu sekondari amefia katika hospitali ya mkoa wa Singida.

Daktari Banubasi amesema majeruhi kumi wamepatiwa huduma ya kushonwa sehemu mbalimbali za miili yao na wanaendelea na matibabu ,pia hakuna majeruhi ambaye atapatiwa rufaa.

Mmoja wa majeruhi akiongea kwa shida huku akiwa amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Singida bwana Ramadhani Mlenga amesema gari halikuwa katika mwendo wa kasi na gafla likaacha njia na kupinduka mara tatu.. 
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger