Sunday 29 June 2014

MWENYEKITI WA CCM KATA YA BUSAMBALA BUTIAMA afariki dunia-baada YA MAJAMBAZI KUMUUA

...

Watu  wanadhaniwa  kuwa ni majambazi wamemuua kinyama kwa kupiga  risasi moja ya kichwani mwenyekiti  wa chama cha mapinduzi  kata ya Busambala wilayani Butiama mkoani Mara Bw Willison Opio mwenye umri wa miaka 6o huku kichwa chake kikisambaratishwa  kabisa na risasi hiyo.


Mauaji hayo ya  kinyama yamefanyika saa saba usiku wa kuamkia leo,baada ya majambazi hayo kuvunja milango ya nyumba aliyokuwa  amelala  kiongozi huyo na familia yake  katika kijiji cha Kwikuba kabla ya kumshambulia kwa bapa za panga mke wamarehemu Bi Agness Wambura  ambaye  alilazimika  kuwapa  kiasi cha shilingi laki nne  ambazo alizikopa kutoka katika taasisi moja ya fedha.

Afisa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Mara Acp Rogati  Mlashan,akizungumza na ITV akiwa eneo la tukio, amesema baada ya majambazi hayo kuvunja  milango  miwili ya nyumba hiyo, walipiga risasi tatu na moja kumpata  kichwani kiongozi huyo wa CCM na kufariki  dunia  papo hapo na kusema kuwa jeshi la polisi  litafanya kila  liwezavyo  ili kuhakikisha wote walihusika kufanya uhalifu huo  wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria. 

Kwa upande  wao  baadhi ya  viongozi  serikali katika  kata ya Busambala,wakizungumzia tukio hilo pamoja na kuonyesha masikitiko yao baada ya kupata taarifa za kifo cha kiongozi huyo wa CCM,wameliomba jeshi la polisi kuendesha msako mkali ambao  utawesha kukamatwa kwa  wahusika,hatua ambayo wamesema itasaidia kuondolea wananchi hofu kubwa waliyonayo sasa. 
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger