Saturday 28 June 2014

MWANAMKE ASALIMISHA SHANGA ZA MAJINI KANISANI SOMA HAPA

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mwanamke anayefahamika kwa jina la Asnath Terevaeli akikabidhi shanga kwa Mchungaji Kiongozi, (Frank Endrew) wa Kanisa la Ufufuo na Uzima mkoani Arusha.Katika hali ya kushangaza, mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Asnath Terevaeli hivi karibuni aliamua kukabidhi kanisani shanga za majini kwa kile alichodai kuwa, zimekuwa zikimtesa na kumfanya akose amani.
Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita katika Kanisa la Ufufuo na Uzima mkoani hapa baada ya moto wa Injili kuwashwa na Mchungaji Kiongozi, Frank Endrew.
Akizungumza na Risasi Jumamosi, mmoja wa waumini wanaosali kanisani hapo aliyejitambulisha kwa jina la Yusta John alisema, awali mwanamke huyo alionekana mwenye jambo linalomtatiza na lilipotolewa tangazo la wenye matatizo kupita mbele, Asnath alifanya hivyo huku akiwa ameshika shanga mkononi.
“Watu wengi walikuwa na shauku ya kujua lililomsibu mama huyo lakini alipofika alimkabidhi mchungaji Frank shanga hizo zilizotengenezwa kiasili zinazodaiwa ni za majini.
Shanga zilizosalimishwa.
Shanga zilizosalimishwa.
“Mwenyewe alieleza kuwa, alipewa kama zawadi na mwanaye lakini cha ajabu zimekuwa zikimtesa na kumfanya akose amani.
 Mchungaji Gwajima
Mchungaji Gwajima
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger