WAKATI wanaharakati wanaendelea kupiga kelele kuhusu kushamiri kwa
vitendo vya unyanyasaji kwa watoto duniani kote, mwanamke aliyetajwa kwa jina la Amina Hamis, mkazi wa Kata ya Kwembe, Malamba Mawili Kitongoji cha Mpakani, Kinondoni jijini Dar ametiwa mbaroni kwa madai ya kumuua kwa kipigo mtoto Munili Omar (6).

UWAZI LATINGA ENEO LA TUKIO
Awali, habari za madai ya mtoto huyo kuuawa yalitua kwenye chumba cha habari cha Uwazi ambapo mwandishi wetu alifunga safari hadi eneo la tukio.
Mtu wa kwanza kuonana naye alikuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, James Nyanda ambaye alikiri kutokea kwa mauaji hayo ya kikatili.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu mkasa mzima wa mtoto huyo, mwenyekiti huyo alisema:
“Ilikuwa saa 2 asubuhi ya Juni 19, nikiwa nyumbani kwangu nilipigiwa simu na msamaria mwema na kunifahamisha kwamba nyumbani kwa Juma Omar kulikuwa na msiba wa kutatanisha uliotokea jana yake, yaani Juni 18 asubuhi.

“Niliuliza sababu ya kukaa na maiti hiyo ndani kwa siku nzima bila kuipeleka hospitali, nikajibiwa alikuwa akimsubiri mumewe ambaye hakuwepo.

“Alipotoa kauli ile nilishangaa sana, nikamwambia arudi nyumbani kwa sababu tusingeweza kumzika mwanaye bila yeye kuwepo, akasema atarudi.”

Mwenyekiti huyo aliendelea kusema: “Kutokana na utata wa kifo hicho niliamua kuwapigia simu polisi wa Kituo cha Mbezi Kwayusuf ambao walifika, wakamchukua Amina, wifi yake na mwili wa mtoto huyo wakaupelea kuuhifadhi Hospitali ya Tumbi (Kibaha) kisha mama huyo kushikiliwa kituoni kumsubiri mumewe.
“Mume ambaye hakujua kiini cha kifo cha mwanaye alipowasili aliunganishwa na mkewe kituoni lakini polisi walishindwa kuwa na ushahidi wa mtoto huyo kuuawa hivyo waliandika RB ya KIFO CHA UTATA kisha wakaruhusiwa kurudi nyumbani kuandaa taratibu za mazishi ya mtoto wao,” alisema mwenyekiti.

Mwenyekiti huyo aliendelea kusimulia kwamba, kufuatia akina mama wa Kitongoji cha Mpakani kutilia shaka kifo cha mtoto huyo waliyedai alikuwa akinyanyaswa na kupigwa mara kwa mara, kurushwa kichura, kufungiwa ndani, kunyimwa chakula, kukataa kumpeleka hospitali kwa madai angelazwa jambo ambalo hakuhitaji kulisikia, waliamua kumbana wifi yake Faudhia, ndipo akaweka wazi kwamba kifo chake kilitokana na kipigo!!!
Kwa mujibu wa maelezo ya Faudhia, siku ya tukio, marehemu Munili ambaye mama yake mzazi anaishi Nzega, Tabora, alikojoa kitandani ndipo mtuhumiwa akampeleka sebuleni na kuanza kumchapa mwilini na kichwani hadi akakata roho mbele yake.

FAUDHIA ALIFUNGUKIA UWAZI
Akizungumza na Uwazi msibani hapo, Faudhia alisema:
“Siku ya tukio ambayo ilikuwa Juni 18, Munila alikojoa kitandani ndipo wifi alimtoa sebuleni na kuanza kumchapa kwa kutumia mkanda. Alipoona mtoto ametulia, aliniita na kuniambia Munili alianguka hivyo niende nikamwite nesi anayemiliki duka la dawa mtaani, nilimwona Munili akitokwa povu mdomoni, jeraha la kupigwa na mkanda kwenye paji la uso na shingoni, nilipomuuliza alipatwa na nini akaniambia alianguka.
“Nilipofika kwa nesi akaniambia kama mtoto alizidiwa tumpeleke
hospitali, nilirudi nyumbani na kumweleza wifi, ndipo akachukua maji ya
baridi na kummwagia Munili lakini hakuamka, alichukua kitenge akampepea
lakini Munili alitulia kimya.Akizungumza na Uwazi msibani hapo, Faudhia alisema:
“Siku ya tukio ambayo ilikuwa Juni 18, Munila alikojoa kitandani ndipo wifi alimtoa sebuleni na kuanza kumchapa kwa kutumia mkanda. Alipoona mtoto ametulia, aliniita na kuniambia Munili alianguka hivyo niende nikamwite nesi anayemiliki duka la dawa mtaani, nilimwona Munili akitokwa povu mdomoni, jeraha la kupigwa na mkanda kwenye paji la uso na shingoni, nilipomuuliza alipatwa na nini akaniambia alianguka.

Faudhia aliongeza kuwa, alipowaeleza ukweli akina mama kuhusiana na tukio hilo, wifi yake alitoka ndani na kutaka kutoroka lakini walifanikiwa kumnasa ndipo nilichukuliwa mimi, kaka (baba wa marehemu), tukapelekwa tena polisi ambako nilieleza kilichotokea, wakaamua kuwashikilia wao hadi leo (Juni 21, mwaka huu).
KAMANDA WA POLISI AZUNGUMZA
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura alipopigiwa simu na kuulizwa kama alikuwa na taarifa ya mauaji hayo alisema hakuwa na taarifa ila atafuatilia.
0 comments:
Post a Comment