“Huo ulikuwa ni Mdundiko wa kawaida, tokea zamani tulikuwa hatuombi kibali na wao walifanya hivyo kama mila zinavyosema, siku ya tukio Juni 18, mwaka huu hatukuwa na sherehe hapa nyumbani isipokuwa jana yake ndiyo kulikuwa na sherehe ya kumpa zawadi mwanangu.
Kwa upande wake majeruhi Grace Loy (20), mkazi wa Mwananyamala Mchangani, alisema anachokijua ni kwa alipigwa risasi katika paja la kulia wakati huo wa vurugu ya kuwataka watawanyike.
“Sisi tulikuwa tukiwasindikiza watu wa tarumbeta ambao walikuwa wanaume, tuliobaki tulikuwa wanawake na hakukuwa na vurugu wala hatukumpiga askari ila sisi tumepigwa risasi kama swala,” alisema Grace.
Majeruhi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Zawia Hamis (20), mkazi Mwananyamala anayedai kupigwa risasi tumboni na kwenye makalio, alisema ameshangazwa na kitendo hicho.
Walisema ni jambo la ajabu kuwa polisi walitumia nguvu kubwa dhidi ya wanawake waliokuwa hawana silaha yoyote.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Makumbusho, Husna Nondo alisema watu hao hawakuwa na kibali cha aina yoyote na kusisitiza kuwa serikali imeshapiga marufuku ngoma za Kanga Moko hivyo amewataka wananchi kufuata agizo hilo la serikali.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura alipoulizwa juu ya suala hilo, alisema upelelezi unaendelea ili kubaini tatizo.
0 comments:
Post a Comment