Monday 23 June 2014

"KONDOMU" ZANASWA UKUMBI WA BUNGE,SPIKA ASHITUSHWA

...

Inaweza kuonekana ni kituko cha aina yake, lakini ni kweli kimetokea kwenye Ukumbi wa Bunge la Kaunti ya Nairobi na kuwaacha wabunge vinywa wazi. 
Katika hali isiyo ya kawaida,
boksi la kondomu lilikutwa ndani ya ukumbi huo na kuwashtua wabunge wote akiwamo spika wa bunge hilo.
Mwakilishi wa eneo la Karura, Kamau Thuo ndiye aliyekuwa wa kwanza kuliona boksi hilo na kuwashtua wabunge wengine hali iliyoibua mjadala mzito.
Kutokana na sintofahamu hiyo Spika Alex Ole Magelo aliwataka wahudumu kufungua boksi hilo kujua kilichomo ndani yake ndipo walipokuta kondomu.
ndomu
“Nafahamu wote humu ni watu wazima, lakini ninachoshangaa ni nani ambaye ameleta kondomu hizi ndani ya ukumbi huu,” alihoji Spika Magelo.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Afya, Manoah Mboku aliwaondoa hofu wabunge na kueleza kuwa kondomu hizo zilipaswa kuwekwa kwenye vyoo vya wanaume hata hivyo kwa bahati mbaya zikapelekwa mahali kusikohusika.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger