Thursday 19 June 2014

Marehemu Kanali(mstaafu) Ally Hassan Mwanakatwe aagwa Lugalo

...

Kanali Ally Hassan Mwanakatwe alizaliwa tarehe 05 Julai, 1949 katika Kijiji cha Dareda, Kata ya Dareda, Tarafa ya Dareda, Wilaya ya Babati katika Mkoa wa
Manyara. Alisoma Shule ya Msingi Singe Wilaya ya Mbulu aliyohitimu kuanzia mwaka 1954 hadi mwaka 1962 na baadaye kujiunga na Shule ya Sekondari Kigonsera akiwa Mtahiniwa Binafsi kuanzia mwaka 1969 hadi alipohitimu Kidato cha Nne mwaka 1972. Alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa tarehe 14 Septemba, 1964 kwa kujitolea kwa muda wa miaka mitatu (3). Alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tarehe 01 Julai, 1967 na kutunukiwa Kamisheni katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tarehe 01 Julai, 1975. Marehemu alistaafu utumishi Jeshini tarehe 04 Julai, 2006 akiwa amelitumikia Jeshi kwa muda wa miaka 39 na siku 4.

Katika utumishi wake Jeshini, Marehemu Kanali Ally Hassan Mwanakatwealihudhuria kozi mbalimbali ikiwemo kozi ya Afisa Mwanafunzi, Tanzania, 1975, Kozi ya Organization, Israel, 1967, Stashahada ya Uhasibu, Tanzania, 1968, Kozi ya Kamanda Patuni, Tanzania, 1977, kozi ya Kamanda Kombania,Tanzania, 1982, Shahada ya Kwanza ya Sanaa, Tanzania, 1982, Masters of Arts in Public Administration, Tanzania, 1985, Kozi ya Ukamanda na Unadhimu Canada 1988, Kozi ya Uangalizi wa Amani Tanzania, 1994.
Marehemu Kanali Ally Hassan Mwanakatwe wakati wa utumishi wake Jeshini alishika madaraka mbalimbali  ikiwemo Mkufunzi, Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa, 1969 – 71, Afisa Mnadhimu Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa, 1977 – 78, Kamanda Kombania, Vita vya Kagera, 1978 – 79,  Msaidizi wa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, 1983 – 84, Muhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1984 – 87, Mkufunzi Mkuu Msaidizi Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Maafisa, 1988 – 91, Afisa Mnadhimu, Makao Makuu ya Jeshi, 1991 – 92, Mkufunzi High Commanders Training Wing, 1992 – 95, Katibu Mkuu, Chama cha Mpira Tanzania (FAT), 1993 – 97, Mkurugenzi wa Elimu, Makao Makuu ya Jeshi, 1998 – 2001, Afisa Mnadhimu, Baraza la Usalama la Taifa, 2001 – 04, Mkurugenzi wa Makumbusho, Makao Makuu ya Jeshi, 2004 hadi alipostaafu utumishi Jeshini tarehe 04 Julai, 2006.
Kwa kutambua na kuthamini mchango wake katika kulitumikia Jeshi na kulinda Taifa, Rais na Amiri Jeshi Mkuu alimtunuku medali mbalimbali zikiwemo medali ya Vita vya Kagera, Miaka 20 ya JWTZ, Miaka 40 ya JWTZ, Utumishi Mrefu Tanzania, na  Utumishi Uliotukuka Tanzania.
Marehemu Kanali Ally Hassan Mwanakatwe alifariki dunia tarehe 07 Juni, 2014 katika Hospitali ya Jeshi Lugalo alikopelekwa kwa matibabu.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, amin.
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) wakibeba jeneza lenye mwili wa Marehemu Kanali (Mstaafu) Ally Hassan Mwanakatwe  katika hospitali kuu ya Jeshi, lugalo Dar es Salaam.

Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Kanali (mstaafu) Ally Hassan Mwanakatwe katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Jeshi Lugalo.
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger