Sunday 22 June 2014

KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU PROFESA MCHOME AZINDUA OFISI ZA NACTE MIKOANI

...


Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome (kulia) akimkabidhi Edward Mneda nyaraka za utendaji kazi kufuatia kuteuliwa kuwa Mkuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Kanda ya Kati. Kushoto ni Mkuu wa Kanda Msaidizi wa Kanda ya Ziwa Beatrice Mpanda. Baraza hilo limefungua ofisi katika kanda tano Dodoma, Arusha, Zanzibar, Mbeya na Mwanza kurahisisha utekelezaji wa majukumu yake.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome (kulia) akimkabidhi Rainey Mwinuka nyaraka za utendaji kazi kufuatia kuteuliwa kuwa Mkuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Kanda ya Ziwa. Katikati ni Katibu Mtendaji wa NACTE Dk. Primus Nkwera na kushoto ni Mkuu wa Kanda Msaidizi Beatrice Mpanda. Baraza hilo limefungua ofisi katika kanda tano Dodoma, Arusha, Zanzibar, Mbeya na Mwanza kurahisisha utekelezaji wa majukumu yake.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji mbalimbali wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) wakiwemo Wakuu Wapya wa Kanda Tano za Baraza hilo muda mfupi baada ya kuzindua rasmi kanda hizo jijini Dar es salaam. Wa tatu kushoto ni Katibu Mtendaji wa NACTE Dk. Primus Nkwera. Ofisi za kanda zilizozinduliwa ni Arusha (Kaskazini), Dodoma (Kati), Mwanza (Ziwa), Mbeya (Kusini) na Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome (kushoto) akibadilishana mawazo na mafias wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi tano za kanda za baraza hilo kwa lengo la kuharisisha utoaji huduma na usimamizi wa vyuo vya ufundi nchini. Kanda hizo ni Kaskazini (Arusha), Kati (Dodoma), Ziwa (Mwanza), Kusini (Mbeya) na Zanzibar.
*       Ni utekelezaji wa azima ya kuwa karibu na wananchi
*       Ahimiza uadilifu kwenye uwajibikaji
*       Ataka zitumke pia kuwahudumia wanafunzi wa Elimu ya Juu
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kupitia Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi - NACTE imefungua ofisi tano za kanda ikiwa ni sehemu ya mkakati wa wizara ya kuwekeza katika eneo la usimamizi wa sekta ya elimu nchini ili kuongeza ufanisi na kufikia matokeo makubwa sasa (BRN).
Ofizi hizo na makao yake makuu kwenye mabano ni Kanda ya Kaskazini (Arusha), Kanda ya Ziwa (Mwanza),   Kanda ya Kusini (Mbeya), Kanda ya Kati (Dodoma) na Zanzibar.
Akizindua rasmi kanda hizo JIJINI Dar es salaam mwishoni mwa wiki sanjari na kukabidhi majukumu ya kiutendaji kwa wakuu wa kanda hizo Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome amesema kuanzishwa kwa kanda hizo ni wazi kutaongeza ufanisi na usimamazi wa elimu ya ufundi nchini ambayo ukuaji wake umekuwa ni wa kasi.
Profesa Mchome amesema serikali inatambua uhitaji na mchango wa elimu ya ufundi katika kutoa fursa kwa vijana kupata mafunzo ya stadi za kazi kwenye fani mbalimbali na hivyo kuwezesha upatikanaji wa nguvu kazi inayohitajika na kuwajengea vijana uwezo wa kujiajiri.
Amesema Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itaendelea kutekeleza mikakati iliyojiwekea ya kuhakikisha ubora wa elimu nchini unaismamiwa vema na unalindwa hiyo ikiwa ni pamoja na kukabiliana na watoa huduma kwenye sekta ya elimu wasiokuwa makini
"Tumeanzisha ofisi hizi za kanda ili kuwa karibu na wadau ikiwemo wananchi na watoa elimu ya ufundi tukiamini kuwa usimamizi wa karibu utasaidia kulinda hadhi na ubora wa elimu ya ufundi na pia kuw ana mfumo wenye kutoa majawabu ya haraka na kwa wakati ya changamoto pale zinapojitokeza."Alisema Profesa Mchome
'Ni shabaha ya serikali kupitia Wizara ya Elimu kuhakikisha viwango vya ubora wa elimu yetu katika ngazi mbalimbali unakuwa imara na wenye kukidhi mahitaji ya soko la ajira na kujiajiri ili kuiwezesha sekta ya elimu kuendelea kutoa mchango uanokusudiwa kwenye manedleoe ya kiuchumi na kijamii kupitia rasilimali watu. Kwetu sisi hili ni jambo la msingi na ambalo tutaendelea kuwekeza humo kulinda elimu yetu."Aliongeza Profesa Mchome
Profesa Mchome amesema pamoja na wizara kuwa na shabaha yake katika kuanzisha ofisi hizo za kanda za NACTE ofisi hizo zitachangia pia kutatua changamoto kadhaa ambazo wananchi wamekuwa wakikabiliana nazo katika kufikia huduma kutokana na kukosekana kwa ofisi mikoani.
Amesema utamaduni wa kutegema ofisi zilizopo makao makuu Dar es salaam unapaswa kurekebishwa ili kuwawezesha wananchi kupata huduma katika sekta ya elimu kwa ukaribu zaidi jambo ambalo litawapunguzia pia gharama
"Wizara inatambua ,kuwa mahitaji ya wananchi kwenye taasisi za elimu ni kubwa na hivyo itaendelea kuhamasisha taasisi zilizo chini yake kuwa na ofisi za kanda ili kuwezesha upatikanaji rahisi wa huduma."Alisema Profesa Mchome
Katika hatua nyengine, Profesa Mchome ameaigiza kuwa ofisi hizo za kanda za NACTE zitumike pia kuwahudumia wadau wa elimu ya juu ikiwemo wanafuzni wa elimu ya juu wakati Tume ya Vyuo Vikuu - TCU nayo inapojipanga kuanzisha ofisi za kanda.
Amesema wale wote wanaohitaji msaada na huduma na za Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU) ikiwemo suala la uombaji udahili n.k wanaweza kufika kwenye ofisi za Kanda za NACTE ili kupata msaada wanaouhitaji badala ya kusafiri kwenda Dar es salaam zilipo ofisi za TCU
"Nataka kwa wakati huu ambapo TCU inajipanga na yenyewe kuwa na ofisi mikoani, ofisi hizi za kanda za NACTE zitumike pia kuhudumia wanafunzi wa vyuo vikuu na wa taasisi za elimu ya juu nchini ikiwemo uombaji wa nafasi za kujiunga na vyuo na shughuli nyengine za TCU. Ni imani yangu kwamba agizo hili litafanyiwa kazi ili kuwaondolea wananchi usumbufu wa muda na wa gharama wanaolazimika kufuata huduma za TCU Dar es salaam." Alisema
Profesa Mchome amewataka wakuu walioteuliwa kuongoza ofisi hizo kuhakikisha wanawatumikia wananchi na wadau kwa uadilifu ili lengo la Wizara la kuwa karibu na wananchi liweze kutimia na kutoa tija inayokusudiwa.
Kwa upadne wake Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi - NACTE Dk Primus Nkwera amesema ofizi hizo za kanda zitakuwa na majukumu ya kusimamia na kutekeleza mipango na mikakati ya Baraza na Wizara kwa ujumla katika sekta ya elimu ya ufundi nchini ikiwemo udhibiti na usimamizi wa vyuo vya elimu ya ufundi.
Aidha, Dk. Nkwera amesema ofisi hizo tayari zimeshapangiwa wkauu wake ambao wanaanza kazi mara moja
"Wadau   wote walio jirani na mikoa hiyo wanaweza kupata huduma zetu zote pasipo kulazimika kuja Dar es Salaam. Pia waombaji wote wa programu za shahada wanaoendelea kutuma maombi yao kwa njia ya mtandao wanashauriwa kuwasiliana na ofisi za kanda kwa kupata msaada wa haraka zaidi pale wanapokutana na matatizo ya kiufundi."Alisema Dk. Nkwera
Kuzinduliwa kwa ofisi hizo kunakuja wakati ambapo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imejikita katika utekelezaji wa programu mbalimbali zenye lengo la kufikia na kutoa matokeo makubwa chini ya mkakati mkuu wa serikali wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ambapo sekta ya elimu ni moja ya sekta kuu sita zinazopewa kipaumbele kwenye BRN.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger