Monday 23 June 2014

MTOTO MWENYE UMRI WA MWAKA MOJA ATELEKEZWA NA MAMA YAKE

...
VITUKO uswahilini! Mtoto wa mwenye umri umri wa mwaka mmoja ambaye jina halikufahamika ameokolewa na Oparesheni Fichua Maovu ya Global Publishers baada ya kudaiwa kutelekezwa kwa siku nzima na mama yake mzazi, Mama Sofia.
Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja aliyetelekezwa na mama yake.
Tukio hilo la aina yake lilijiri Juni wikiendi iliyopita maeneo ya Somanga-Magomeni, Dar ambapo kwa mujibu wa wasamaria wema waliomuona mtoto huyo, alionekana majira ya asubuhi akirandaranda barabarani.
Walisema walidhani alikuwa akielekea nyumbani kwao lakini hadi jioni walishangaa kumuona bado anarandaranda mitaani mwenyewe.
Mtoto huyo akiwa na msamaria.
Baadaye OFM ilipewa taarifa na kufika eneo la tukio ambapo ilipata maelezo kuwa mama wa mtoto huyo huwa na tabia ya kumwacha mwanaye mara kwa mara mtaani bila kumjali.

OFM ilifikisha suala hilo kwa mjumbe wa mtaa huo ambaye alimtambua mtoto huyo mara moja kwa kuwa alikuwa akiishi naye nyumba moja hivyo alimpeleka kwa wazazi wake huku akiwapa onyo kali.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger