Sunday 22 June 2014

VYAMA VYA SIASA TANZANIA VYAIPINGA NEC

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

http://freemedia.co.tz/daima/wp-content/uploads/2014/06/nccr.jpg
Hatua ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuandika upya daftari la kudumu la wapiga kura, imeendelea kupingwa kwamba haijavishirikisha vyama vya siasa nchini kama wadau muhimu.Katika mahojiano na Tanzania Daima Jumapili, Katibu Mkuu wa NCCR – Mageuzi, Mosena Nyambabe, alisema NEC itegemee changamoto nyingi kujitokeza katika mchakato ambao wameupanga na Serikali ya CCM.

"NEC haikutakiwa kufundishwa kwamba ikae na wadau katika mchakato huu. Inajua kabisa kabla ya uchaguzi mkuu wowote wanapaswa kuboresha daftari kwa kushirikiana na wadau, inakuwaje sasa wameamua kufanya peke yao?" alihoji Nyambabe. 
Alisema kama wadau wangeshirikishwa jambo hilo wasingekubaliana na NEC kutumia teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration (BVR) kutoa vitambulisho ambayo alidai imesababisha matatizo mengi katika chaguzi za nchi za Afrika.
"Nchi za Afrika kama Ghana, Zambia, Malawi, Afrika Kusini na nyingine nyingi zimekuwa na ugomvi mkubwa kati ya tume zao za uchaguzi na vyama vya siasa wakati wa kujumlisha na kutoa matokeo," alisema.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Bukoba, Dk. Azaveli Lwaitama, alihoji ni kwanini serikali kupitia NEC itoe taarifa hiyo muhimu pasipo kuwashirikisha wadau ambao ndio wateja wao.
"Sidhani kama serikali ina nia ya dhati ya kuandikisha upya daftari la kupiga kura kwa Watanzania. Kama walikuwa nayo, walipaswa kuwashirikisha wadau kwa ajili ya kupata maoni ili kuondoa kelele nyingi wakati wa uchaguzi," alisema.
Dk. Lwaitama alisema kitendo cha NEC kutumia mfumo wa BVR ambao umekuwa ukikosolewa na wadau katika nchi za Afrika ni hatari.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger