Thursday 19 June 2014

UTARATIBU WA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO 2014

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) imetangaza 
majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka 2014 ambao 
waliomaliza kidato cha nne mwaka 2013

Wanafunzi waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti kwenye shule walizopangiwa kuanzia tarehe 10 Julai 2014
 na mwisho wa kuripoti ni tarehe 30 Julai 2014. Aidha, hakutakuwa na mabadiliko ya wanafunzi kubadilishiwa 
shule walizopangiwa, hivyo wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangiwa kama
 inavyoonekana katika matokeo haya.

TAARIFA:

Uchaguzi wa wanafunzi wa kuingia Kidato cha Tano katika shule za  Serikali na Vyuo vya Ufundi kwa
 mwaka 2014 umekamilika. Uchaguzi umefanyika kwa kuzingatia takwimu za matokeo ya watahiniwa
 waliofanya Mtihani wa Kidato cha Nne Tanzania Bara mwaka 2013.

2.0 WATAHINIWA WALIOFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE, MWAKA 2013

Jumla ya watahiniwa  427,679  walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2013, wakiwemo
 wasichana  199,123  sawa na asilimia  46.56  na wavulana  228,556 sawa na asilimia  53.44. 
Kati yao watahiniwa  404,083  sawa na asilimia  94.48  walifanya mtihani na watahiniwa  23,596 
 sawa na asilimia  5.52  hawakufanya mtihani huo.

2.1 Watahiniwa wa Shule (School Candidates)

Kwa Watahiniwa wa Shule, watahiniwa  367,163  walisajiliwa kufanya mithanikati yao wavulana ni
 198,099  na wasichana ni  169,064.  ambapo  watahiniwa  352,614 sawa na asilimia  96.04 
walifanya mtihani; kati yao wasichana walikuwa 162,412 sawa na asilimia  96.07  na wavulana
190,202  sawa na asilimia  96.01 . Watahiniwa 14,549  sawa na asilimia  3.96  hawakufanya mtihani
 kwa sababu mbalimbali.

2.2 Watahiniwa wa Kujitegemea (Private Candidates)

Kati ya watahiniwa 60,516  wa kujitegemea waliosajiliwa kufanya mtihani, watahiniwa  51,469 
 sawa na asilimia  85.05 walifanya mtihani na watahiniwa  9,047  sawa na asilimia  14.95  hawakufanya
 mtihani kwa sababu mbalimbali.

Jumla ya watahiniwa  235,227  sawa na asilimia  58.21  ya watahiniwa waliofanya Mtihani wa Kidato
 cha Nne 2013 walifaulu. Mwaka 2012 watahiniwa waliofaulu walikuwa  185,940  kati ya  431,650 
 waliofanya mitihani; hii ni sawa na asilimia  43.08.  Matokeo haya yanaonesha kuwa mwaka 201
3 ufaulu umeongezeka kwa asilimia  15.13.

3.1 Ufaulu wa Watahiniwa wa Shule

Mwaka 2013 Watahiniwa wa Shule waliofaulu ni  201,152  sawa na asilimia  57.05  ya watahiniwa
352,614  waliofanya  mtihani.  Kwa mwaka 2013 kuna ongezeko la ufaulu wa watahiniwa 41,405, 
sawa na asilimia 25.91 ikilinganishwa na ufaulu wa mwaka 2012 ambapo watahiniwa 159,747
 walifaulu.

3.2 Ufaulu wa Watahiniwa wa Kujitegemea

Takwimu zimeonesha kuwa kumekuwa na ongezeko la ufaulu kwa watahiniwa wa kujitegemea kutoka
 26,193,  sawa na asilimia  43.07  mwaka 2012 hadi kufikia watahiniwa  34,075,  sawa na asilimia
66.21  kwa mwaka 2013; Kwa kulinganisha na mwaka 2012 lipo ongezeko la asilimia  30.09 kwa
 ufaulu wa watahiniwa wa kujitegemea.

Ufaulu wa watahiniwa wa shule kwa mwaka 2013 katika madaraja ya I -III umefikia watahiniwa
 71,527  sawa na asilimia  20.28  ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara. Hivyo
 kuna ongezeko la ufaulu wa asilimia  106.73  ikilinganishwa na matokeo ya ufaulu kwa mwaka
2012, kwa kuwa watahiniwa wa shule waliofaulu katika madaraja I-III kwa mwaka huo walikuwa
34,599  sawa na asilimia  9.67  ya watahiniwa waliofanya mtihani.

5.0 TARATIBU ZA UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO 2014.

Kulingana na utaratibu uliowekwa na Serikali, mwanafunzi anayeomba kuchaguliwa kuendelea na
elimu ya sekondari kidato cha tano na vyuo vya Ufundi, hulazimika kujaza  ‘Selform'  ambayo ndiyo
 fomu rasmi ya maombi. Kwa kutumia fomu hiyo, mwanafunzi huchagua maombi  matano ya tahasusi 
(Combinations) za masomo anayotaka kusoma na shule anayotarajia kujiunga nayo kwa kila chaguo.
Kamati ya uchaguzi humpanga mwanafunzi katika machaguo yake ya  masomo na shule kwa kuanzia

 na chaguo la kwanza. Kama mwanafunzi atakuwa hana sifa katika machaguo yote aliyoomba,
 mwanafunzi husika hupangiwa chaguo la somo alilofaulu zaidi na katika shule iliyopo karibu na
 wilaya yake ya makazi kulingana na tahasusi na nafasi zilizopo katika shule husika.

6.0 IDADI YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUINGIA KIDATO CHA TANO

Jumla ya Wanafunzi  54,085  sawa na asilimia  75.61  ya wanafunzi  71,527  waliostahili kuingia
 Kidato cha Tano Tanzania Bara kwa mwaka 2014 wamechaguliwa; hilo ni ongezeko la wanafunzi
  20,402  kwa kulinganisha na wanafunzi  33,683  waliochaguliwa mwaka 2013. Kati ya wanafunzi
 waliochaguliwa 2014 wavulana ni  31,352 na wasichana ni  22,733.

Wanafunzi wamechaguliwa kujiunga kidato cha Tano katika jumla ya shule  241  zikiwemo shule
 33  zilizopangiwa wanafunzi kwa mara ya kwanza mwaka 2014.

Nawashukuru sana wadau wote wa elimu katika Halmashauri mbalimbali kwa kuimarisha miundombinu
 ya shule hizo, ikiwemo maabara.

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha Tano 2014 ni kutoka shule za serikali na zisizo za
serikali. Kati yao wavulana  14,826  sawa na asilimia 27.41 wamechaguliwa kusoma masomo ya
 sayansi  na wavulana  16,526  sawa na asilimia  30.56  wamechaguliwa kusoma masomo ya  sayansi
 ya Jamii.  Aidha,wasichana  7,859  sawa na asilimia  14.53 wamechaguliwa kusoma masomo ya
 sayansi  na wasichana  14,874  sawa na asilimia  27.50  wamepangwa kusoma masomo ya  Sayansi ya
 Jamii.

Nawapongeza walimu wote kwa juhudi walizozifanya katika ufundishaji kwa kuzingatia mbinu za
 ufundishaji walizopata kupitia mpango wa mafunzo kazini  (INSET) kwa walimu wa sayansi na lugha
(Kiswahili na Kiingereza) unaosimamiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na
Ofisi ya WaziriMkuu, Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa. Aidha nawapongeza wanafunzi wote
 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi. Hali hiyo inaonesha kuwa jitihada
za Serikali za kuhamasisha vijana kusoma masomo ya Sayansi zimeanza kuzaa matunda.

Natoa wito kwa wanafunzi wa  jinsi zote  kujisomea kwa bidii masomo  yote, yakiwemo ya
 Sayans i na  Sayansi ya Jamii , kwani yanategemeana. Walimu wa masomo ya Sayansi, Sayansi
 ya Jamii na Hisabati wanakumbushwa kutumia mbinu shirikishi za  kitaalam na kisaikolojia 
  katika kufundisha ili kuwavutia wanafunzi wengi zaidi kusoma na kufaulu mitihani yao. Aidha
 walimu wa masomo ya Sayansi, waendelee kuwahamasisha wanafunzi kusoma masomo ya Sayansi
 wakiwemo  wanafunzi wa kike . Aidha, wanafunzi wa kike wanapaswa kujiamini kuwa wanaweza
 masomo yote yakiwemo ya Sayansi, kwani siri ya kujifunza ni utayari.

7.0 WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO VYA UFUNDI, MWAKA 2014

Jumla ya wanafunzi  472 wakiwemo wavulana  355 na wasichana  117 wamechaguliwa
kujiunga na Vyuo vya Ufundi. Idadiya wanafunzi hao imepungua kutoka  530  mwaka 2013
hadi  472  mwaka 2014 kwa sababu kwa sasa vyuo hivyo vimeanza kuchukua wanachuo
 wa shahada ya kwanza. Aidha, kutokana na ufaulu kuongezeka idadi ya  wanafunzi 
wa kike  waliochaguliwa kujiunga na vyuo hivyo imeongezeka kutoka wanafunzi  114  mwaka
2013 hadi wanafunzi  117 mwaka 2014 sawa na
 ongezeko la asilimia  2.63.

Natoa wito kwa wanafunzi kuendelea kusoma kwa bidii masomo ya sayansi ili mwakani idadi ya wanafunzi wanaojiunga na mafunzo ya ufundi iongezeke ili Taifa lipate wataalam wa kutosha wa ngazi zote.

8.0  SABABU ZA WANAFUNZI KUKOSA KUCHAGULIWA KUINGIA KIDATO CHA TANO 
 Jumla ya wanafunzi  16,800  wakiwemo  watahiniwa wa kujitegemea 10  waliokuwa na sifa za
msingi hawakuchaguliwa kwa sababu mbalimbali zikiwemo: ufinyu wa nafasi za shule za Kidato cha
 Tano (wanafunzi  16,400 ) na kukosa  tahasusi - Combination  (wanafunzi  400 ).

Serikali inatarajia kufanya uchaguzi wa awamu ya pili baada ya kubaini nafasi zitakazokuwa wazi
zinazotokana na wanafunzi ambao hawakuripoti awamu ya kwanza. Aidha, Serikali imeweka
utaratibu wa kuwapatia nafasi ya kusoma kidato cha Tano na cha Sita kwa pamoja na shahada ya
Ualimu wanafunzi wenye sifa.

Shule za Kidato cha Tano na Sita zinatakiwa kuwa na mahitaji ya msingi, ikiwemo miundombinu
yenye uwiano sahihi wa  vyoo, bafu, vyumba vya madarasa, bweni, jiko, bwalo, maktaba,
 maabara, chumba cha Jiografia ; pamoja na  samani  kulingana na idadi ya wanafunzi.

Shule zenye Kidato cha Kwanza mpaka cha Nne ambazo zinahitaji kuanzisha kidato cha Tano,
zinatakiwa kuwa na miundombinu na mahitaji kamilifu yanayotosheleza kidato cha Kwanza hadi
 cha Nne kabla ya kuanza kujenga miundombinu ya Kidato cha Tano na Sita.

Natoa wito kwa Makatibu Tawala Mikoa wawaelekeze Wakurugenzi wa Halmashauri, Miji na
Majiji kuhakikisha azma ya Serikali ya kila Tarafa kuwa na shule ya Kidato cha Tano inatekelezwa
ili kupunguza idadi ya wanafunzi wanaokosa na
fasi. Kutokana na ongezeko la ufaulu wa masomo ya sayansi tunahimiza shule zitakazoanza Kidato
cha Tano ziwe na maabara ili kuongeza idadi ya
 wanafunzi wa tahasusi za sayansi.

Aidha, shule ambazo hazikupangiwa wanafunzi kutokana na mapungufu mbalimbali,
 Makatibu Tawala wa Mikoa husika wanahimizwa kuwaelekeza Wakurugenzi kusimamia
kwa karibu ukamilishwaji wa shule hizo ili ziweze kupokea wanafunzi wa chaguo la pili (Second selection).

Natumia nafasi hii kuwahimiza wadau wote wa Elimu kuhakikisha kuwa shule zote zinazoanzishwa
 kwa ajili ya kidato cha Tano ziwe za bweni kwa kuwa wanafunzi wa kutwa ni wachache na ni
  lazima watoke eneo husika.  Kwa mfano, mwaka huu shule ya sekondari Buswelu ya mjini
Mwanza imekosa wanafunzi kwa kuwa ni ya kutwa na Mwanza kuna shule 3 za kutwa. Hivyo
 ilikuwa vigumu kupata wanafunzi wa eneo hilo wa kutosheleza shule hizo.

Wakuu wa Shule  wahakikishe kuwa wanafunzi wa kidato cha nne wote wanajaza ‘Selforms'
 kwa umakini na kwa usahihi ili kurahisisha zoezi la uchaguzi. Aidha, wazazi kwa kushirikiana na
 walimu wawaelekeze watoto wao  kuwa na dira , kuwasaidia kusoma kwa malengo na
kufanya machaguo ya tahasusi kulingana na dira walizonazo.

10.0 WANAFUNZI KURIPOTI KATIKA SHULE WALIZOPANGWA

Muhula wa kwanza kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano mwaka huu 2014,utaanza  mwezi Julai
 tarehe 10 . Wanafunzi wamepangwa katika shule zenye miundombinu na walimu kwa
 masomo husika. Aidha, iwapo baadae mapungufu yatajitokeza, wakuu wa shule wameelekezwa
kutoa taarifa kwa uongozi wa Halmashauri husika kuhusu upungufu huo.

Uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano umefanyika kwa kutumia mfumo wa
 kompyuta kwa kuzingatia machaguo ya wanafunzi pamoja na ufaulu hivyo hakutakuwa na mabadiliko
yoyote. Kwa nafasi hii,  naagiza wanafunzi wote kuripoti katika shule walizopangwa tarehe 10 Julai, 
2014 . Wanafunzi ambao watashindwa kuripoti shuleni hadi tarehe 30 Julai, 2014  nafasi zao zitajazwa na
 wanafunzi ambao wamekosa nafasi.

Mwisho ninachukua nafasi hii kuwapongeza wanafunzi waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Tano
 na Vyuo vya Ufundi mwaka 2014, walimu, wazazi, Bodi za Shule, viongozi, jamii na wadau wote
wa elimu kwa jitihada za kuwaandaa wanafunzi, na kufanikiwa kuingia Kidato cha Tano.
Ushirikiano wa wadau wote unatakiwa ili kuboresha elimu hapa nchini.

Wataalam wa elimu kuanzia ngazi ya shule wawe na utaratibu endelevu wa kuelimisha wadau katika
utekelezaji wa malengo yanayopimika. Katika utaratibu wa ”Matokeo Makubwa Sasa  (Big Results Now)
”;  kila mmoja anatakiwa  kuacha utendaji wa mazoea  na afanye kazi  kwa malengo na viwango ,
 kuwa na  mipango inayotekelezeka  ya muda mfupi na muda mrefu na kuwa na  vipindi vya tathmini 
 kwa kila lengo kabla, kati na mwisho wa utekelezaji. Ni matumaini yangu kuwa wakuu wa shule na
viongozi wote wa elimu wakizingatia taratibu hizi, elimu inayotolewa hapa nchini itaendelea kuwa bora zaidi.

Soma Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2014 hapa

Ahsanteni kwa kunisikiliza.
Mhe. Kassim M. Majaliwa (MB)
OFISI YA WAZIRI MKUU - TAMISEMI


© 2015 PMORALG
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger