
MUIGIZAJI ambaye kwa sasa amejikita kwenye muziki, Zuena Mohammed ‘Shilole’ amegandwa na madai ya utapeli kufuatia jamaa mmoja aitwaye Samir kuibuka na kudai kuwa, walimpa shilingi laki mbili ili awakodishie madansa kwa ajili ya video yao lakini mpaka sasa anachenga.
Akijibu tuhuma hizo, Shilole alisema kwa sasa yeye ana uwezo kifedha hivyo hawezi kudhulumu kiasi hicho kidogo cha pesa ila wao wanapowahitaji wacheza shoo wake wakarekodi, yeye anakuwa yuko bize nao.”
0 comments:
Post a Comment