Tuesday 17 June 2014

MWANAMAMA HUYU ACHARANGWA MAPANGA BAADA YA KUVAMIWA NA KIJANA MMOJA,AMBAE NAE AUWAWA

...




Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Jumanne Joel(25-30) ameuawa na
wananchi wenye hasira kali baada ya kumvamia Monica Lutonja(32)  wa kijiji cha Nyankumbu katika kata ya Kalangalala mjini Geita .Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana ambapo inadaiwa kuwa watu watatu akiwemo marehemu walienda kwa mama huyo na kugonga hodi wakidai kuwa wao na rafiki wa kaka yake ambaye ni Bunegezi.Baada ya Monica Lutonja kufungua 


walianza kumkatakata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake hadi kupoteza fahamu.Hata hivyo kelele za mama huyo zilisababisha majirani kutoka na kuanza kuwasaka baada ya kuwa wamekimbia na hatimaye wakamkamata mmoja na wakaanza kumpiga hadi kumuua.Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Joseph Konyo amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa  watuhumiwa wengine wawili bado wanatafutwa na jeshi la polisi kwa ajili ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger