Watu
tisa wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa katika ajali ya gari
iliyotokea eneo la Ifunda mkoani Iringa jana baada ya lori kugonga gari
dogo la abiria aina ya Toyota Hiace.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Amina Masenza alisema dereva wa lori hilo lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam, alishindwa kufunga breki na kuigonga Hiace hiyo iliyokuwa imeegeshwa pembeni ya barabara.
“Lori limeharibika kabisa na Hiace pia imeharibika kabisa,” alisema Kamanda Masenza.
“Lori
hilo liliposhindwa kufunga breki liliigonga Hiace ambalo lilikuwa na
abiria na kwenda mbele na kisha kugonga watembea kwa miguu,,”
Kamanda
Masenza alisema katika ajali hiyo iliyotokea jana jioni, madereva wa
magari hayo wote wamejeruhiwa na wamelazwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa
pamoja na majeruhi wengine.
“Dereva mmoja yupo chumba cha upasuaji kwa kuwa mguu wake umevunjika na mwingine yupo wodini,” alisema
0 comments:
Post a Comment