TANGAZO
BARAZA
LA MITIHANI LA TANZANIA
Baraza
la Mitihani la Tanzania linapenda kuwatangazia watu wote wanaotaka
kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) mwezi, Mei
2015 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba kipindi cha usajili
kilianza rasmi tarehe 1
Julai, 2014 hadi
tarehe
30 Septemba, 2014
kwa ada ya Shilingi 50,000/=.
Aidha kuanzia tarehe 1
Oktoba, 2014 hadi
tarehe 31
Oktoba, 2014
waombaji watajisajili kwa ada ya Shilingi 65,000/-
(ada pamoja na faini).
Waombaji
wote wanasisitizwa
kuhakikisha wanajisajili mapema kwa njia ya mtandao kupitia tovuti
ya Baraza la Mitihani ya www.necta.go.tz.
Kabla
ya kujisajili kwenye mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye vituo
vya mtihani kuchukua namba rejea (reference number) zinazotolewa bure
na kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta au M-pesa.
Imetolewa
Na:
Kaimu
Katibu Mtendaji
Baraza
la Mitihani la Tanzania.
0 comments:
Post a Comment