JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UJENZI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WAZIRI WA UJENZI MHESHIMIWA DKT. JOHN POMBE
MAGUFULI (Mb) KUZURU MIKOA YA MWANZA NA MARA
Wizara
ya Ujenzi napenda kutoa taarifa ka umma kuwa Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli (Mb) anatarajia kufanya ziara ya kukagua miradi mbaimbali ya Maendeleo katika mkoa wa Mwanza na Mara.
Mheshimiwa
Waziri Magufuli ataanza ziara yake Mkoani Mwanza tarehe 06 Julai ambapo
atakagua mradi wa Ujenzi wa barabara ya Usagara – Kisesa (by pass) yenye urefu
wa km. 16.7 inayojenga kwa kiwango cha lami. Siku
inayofata tarehe 07 Julai, Mheshimiwa Waziri ataelekea mkoani Mara kukagua mradi wa barabara ya Makutano – Natta – Mugumu
(sehemu ya Makutano – Sanzate km 50).
Siku
hiyo hiyo mchana Dkt. Magufuli atazindua
rasmi kivuko cha MV. Mara kitakachotoa huduma kati ya Iramba na Majita. Aidha,
baada ya uzinduzi huo Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi atafanya mkutano wa hadhara na kuongea na wananchi wa
eneo la Mwibara ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa mradi wa Barabara ya Nyamuswa – Bunda – Kisorya – Nansio (sehemu ya
Bulamba – Kisorya km 51).
Mheshimiwa
Magufuli ataendelea na ziara yake tarehe 09 Julai Mkoani Mwanza ambapo
atazindua kivuko cha MV. Temesa katika eneo la Nyegezi(Sweya). Kivuko
hicho kimefungwa mitambo ya kukiwezesha kusafiri kwa mwendo wa kasi ili
kukiwezesha kutoa huduma katika mwambao huo wa ziwa Victoria. Aidha, Kivuko
hicho chenye uwezo wa kubeba Tani 65 ambazo ni sawa na abiria 80 na magari
madogo matano kwa wakati mmoja.
Kivuko
hicho kitakuwa kinafanya kazi kutoka Luchelele kupitia Sweya, Butimba, Mkuyuni,
Igogo hadi Kirumba ikiwa ni mkakati wa kupunguza foleni katika jiji la Mwanza.
TAARIFA HII IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO
SERIKALINI WIZARA YA UJENZI
05/07/2014
0 comments:
Post a Comment