Hatua ya
robo fainali ya kombe la dunia inaendelea leo. Saa 1:00 usiku kwa saa za
Afrika mashariki, Ufaransa watachuana na Ujerumani.
Saa 5:00 usiku, wenyeji Brazil watakuwa kibaruani dhidi ya Colombia.
Kfikia sasa hizi ndio takwimu muhimu za kombe la dunia mwaka 2014, nchini Brazil.
Kufikia sasa mpaka michezo 56 kati ya 64 imekwishachezwa,
Takwimu muhimu mpaka sasa,
Mfungaji
bora anayeongoza akiwa ni James Rodrguez wa Colombia mwenye mabao
matano, huku Neymar, Lionel Messi na Thomas Muller wa Ujerumani
wakifuatia wakiwa na mabao manne kila mmoja.
Jumla ya mabao 154 yamefungwa mpaka sasa, ikiwa ni wastani wa mabao matatu kwa kila mechi.
Mechi
iliyoshuhudia mabao mengi zaidi yakifungwa ikiwa ni kati ya Uswiss na
Ufaransa, ambapo jumla ya mabao saba yaliingia wavuni.
Uholanzi
ndo timu iliyofunga mabao mengi zaidi mpaka kwenye michuano hii ikiwa na
jumla ya mabao 12, mabao 11 yakifungwa kwa kupeana pasi huku bao moja
likiwa ni kwa mpira uliokufa.
Ubelgji
ndo timu iliyofanya mashambulio mengi sana langoni mwa timu pinzani,
ikiwa imefanya mashambulizi 81 kwa timu zote ilizokutana nazo, huku
Algeria ikiwa ndo timu iliyokaba sana na kuzuia mashambulizi mengi.
Ujerumani,
Ni mabingwa wa kupiga pasi nyingi zaidi ambapo hadi sasa wamekishapiga
pasi 2560. Ila Javier Macherano wa Argentina ndiye kinara wa kupiga pasi
nyingi zaidi kwa wachezaji, akipiga jumla ya pasi 364.
Michael
Bradely wa Marekani, ni Usain Bolt wa michuano hii akiwa ndiye mchezaji
aliyekimbia sana uwanjani, akikimbia kwa jumla ya mile elfu 54, 709 sawa
na kilometa elfu 88 na 45.
Kwa
upande wa Makipa, Kelya Navas mlinda mlango wa Costa Rica ndiye kipa
aliyeokoa michomo mingi zaidi kwenye michuano ya mwaka huu, ambapo
amekwisha okoa michomo 14 iliyoelekea langoni huku akiruhusu kufungwa
mabao mawili pekee.
Lakini
mlinda mlango wa Nigeria, Austine Edje naye amejiandikia rekodi mpya ya
kuwa mchezaji aliyeitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria
kwenye fainali tatu za michuano ya kombe la dunia lakini hajacheza hata
mechi moja.
Rafael
Marquez wa Mexico amekuwa nahodha aliyecheza fainali nne za michuano ya
kombe la dunia, akianza toka mwaka 2002 nchini Japan hadi sasa Brazil
ambapo timu yake ilitolewa na Uholanzi katika hatua ya kumi na sita
bora.
Akiwa na
umri wa miaka 43 Faryd Mondragon, mlinda mlango wa Colombia amevunja
rekodi ya mkongwe wa Cameroon, Rogger Millar kwa kuwa mchezaji mwenye
umri mkubwa zaidi kucheza mechi za kombe la dunia.
Naye
Kinda wa Marekani anayekipiga kwenye klabu ya Bayern Munich, Julien
Green amekuwa mchezaji wa saba kijana kufunga bao akiwa na umri mdogo
kwenye michuano ya kombe la dunia, akiwa kwenye kundi moja na Lionel
Messi wa Ajentina na Divock Origi wa Ubelgji.
Na
Kwa mara
ya kwanza kwenye michuano ya mwaka huu, vinara wa makundi wamefuzu kwa
hatua ya robo fainali, wakishindwa kufungwa na timu zilizoshika nafasi
ya pili kwenye makundi.
0 comments:
Post a Comment