Watu wawili wamefariki dunia huku wengine watano wakilazwa hospitalini baada kunywa dawa za miti shamba mtaani Karen jijini Nairobi nchini Kenya.
Watu hao saba wanasemekana kunywa dawa hizo walipokuwa wakifanya kazi ya ujenzi wa jengo eneo la Kazuri kule Marula Alhamisi Januari 31,2019.
Waathiriwa walikimbiziwa hospitalini baada ya kulalamika kuhusu maumivu makali kwenye tumbo na kutapika.
Kulingana na taarifa za polisi, mmoja wa waathiriwa aliaga dunia alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Karen na mwingine alifariki akiwa katika zahanati ya St. Odillas.
Waathiriwa wanasemekana kalalama kuhusu maumivu makali kwenye tumbo na kutapika wakati walipofikishwa hospitalini.
Manusura 5 walipelekwa katika hospitali ya St. Mary's ambapo wanapokea matibabu.
"Uchunguzi ulionyesha kuwa walikunywa dawa za miti shamba wakiwa kazini wakifanya ujenzi eneo la Kazuri, maafisa wa polisi walifika eneo la tukio na wakapata jagi iliyokuwa na matawi ya mmea wa Aloe Vera," taarifa ya polisi ilisoma.
Miili ya wawili hao ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhi wafu cha Umash huku maafisa wa polisi wakiendelea na uchunguzi kubaini aliyewapatia dawa hizo.
Via Tuko
0 comments:
Post a Comment