Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM mkoa wa Shinyanga umefanya Bonanza lililohusisha michezo mbalimbali kwa lengo la kusherehekea miaka 42 ya Chama Cha Mapinduzi CCM.
Bonanza hilo limefanyika leo Februari 2,2019 katika uwanja wa mpira wa CCM Kambarage uliopo mjini Shinyanga
Akizindua bonanza hilo mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa amepongeza jitihada zilizofanywa na serikali ya CCM kwa awamu nne zilizopita mpaka sasa awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutekeleza kwa kiwango kikubwa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kupiga hatua za kimaendeleo.
“Vitu vingi vikubwa vimefanyika kupitia CCM na serikali yake na jumuiya zake kwa ujumla, nchi yetu imeendelea kuwa salama miundombinu imeboreshwa barabara ndio usiseme Shinyanga haikuwa hivi, sekta ya afya , elimu vimeboreshwa na tulikuwa na ndege moja leo tunazo saba vyote hivi vipo ndani ya ilani ya chama”alisema Malola
“Na mimi niombe tuendelee kuyaenzi maendeleo haya yaliyoletwa na CCM kwa vitendo”,aliongeza Mlolwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge amewakumbusha vijana kuendelea kudumisha ushirikiano katika mambo yote yanayofanywa na chama pamoja na serikali katika kuleta maendeleo ya wananchi wanaowatumikia.
“Nawashukuru sana ndugu zangu wote na viongozi wote wa serikali na chama mlioshiriki katika Bonanza hili tudumishe umoja na mshikamano kati yetu hivi ndivyo serikali yetu inataka” ,alisema Shemahonge.
Bonanza hilo limeshirikisha michezo mbalimbali ukiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete , mchezo wa kuvuta kamba , kukimbia kwenye magunia na kuwashirikisha viongozi wa serikali na chama cha CCM.
Kauli mbiu kwa mwaka huu inasema “Kazi ni kipimo cha utu ,chapa kazi tulinde uhuru na utaifa wetu”.
Mgeni rasmi katika Bonanza la UVCCM Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza na wadau waliohudhuria katika bonanza la michezo ambapo amepongeza jitihada zilizofanywa na serikali ya CCM kwa awamu nne zilizopita mpaka sasa awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutekeleza kwa kiwango kikubwa ilani ya chama cha mapinduzi kwa kupiga hatua za kimaendeleo. Picha zote na Steve Kanyefu- Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack katika bonanza hilo ambapo aliwataka vijana kushirikiana katika kuijenga Shinyanga wakishirikiana pamoja na serikali yao.
Mwenyekiti UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge (kushoto) akimpatia zawadi ya jezi mgeni rasmi mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa katika ufunguzi wa bonanza hilo.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Husein Egabano akiongoza msafara wa vijana kuingia katika uwanja wa CCM Kambarage lilipofanyika bonanza hilo
Mgeni rasmi katika bonanza hilo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akifungua michezo katika bonanza hilo kwa kupiga penati.
Baadhi ya wadau waliohudhuria katika bonanza hilo wakifuatilia kwa umakini matukio yote yanayoendelea uwanjani.
Timu ya wanawake ambao ni wanachama wa CCM (wenye jezi za kijani) wakichuana vikali na timu ya watumishi wa serikali (wenye jezi za rangi nyekundu) katika mchezo wa pete, ambapo timu ya watumishi ilishinda kwa goli 14 dhidi ya wanachama 9.
Mgeni rasmi mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa( katikati) akiwa pamoja mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba(kulia) pamoja na mwenyekiti UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge (kushoto) wakifuatilia michezo katika uwanja wa CCM Kambarage.
Mpira wa miguu ukiendelea katika uwanja wa Kambarage hapa ni mchezo kati ya timu ya walimu kutoka chuo cha Shy com (wenye jezi ya kijani) na Timu ya Stand United chini ya miaka 20(jezi rangi ya chungwa)
Mgeni rasmi akikabidhi zawadi ya kikombe kwa timu ya watumishi wa serikali walioshinda michezo mingi katika bonanza.
Mchezo wa kukimbia na magunia ukiendelea
0 comments:
Post a Comment