Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Joachimu Kibinda, (48), mchimbaji wa madini na mkazi wa Songambele, wilayani Simanjiro, amefariki dunia baada ya kuangukiwa na kifusi cha udongo akiwa anachimba madini.
Kamanda wa Polisi mkoani Manyara, Augustino Senga, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo jana ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya matukio mbalimbali ambayo yametokea mkoani hapa.
Alisema tukio hilo lilitokea Januari 28 majira ya saa 9:00 alasiri katika maeneo ya Machekecho Machimboni, Kata ya Naisinyai.
Katika eneo hilo, alisema watu wa aina tofauti wanafanya shughuli za uchimbaji wa madini kwa ajili ya kujiingizia kipato.
Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Hai kwa uchunguzi zaidi wa madaktari na taratibu zikikamilika mwili huo utachukuliwa na ndugu zake kwa ajili ya maziko.
0 comments:
Post a Comment