Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara ameibuka kwa mara ya kwanza kufuatia kichapo cha pili mfululizo cha mabao 5-0 dhidi ya Al Ahly ya nchini Misri.
Kupitia ukurasa wake wa Instagrma, Haji Manara amewapa pole mashabiki wa klabu hiyo na kuwapa ahadi kuwa Simba lazima ipate pointi 6 za nyumbani na itafuzu hatua inayofuata ya michuano hiyo.
"Poleni sana Wanasimba wote, Najua mnavyojisikia now ila niwaambie hesabu zipo kwetu,kama ninavyowaambia always,lazima tupate points tisa za nyumbani!! Yes tukifanikiwa kushinda mechi mbili zilizobaki za home,wanaowacharura leo watawapa hongera!! Yes We Can".
Simba imepoteza mchezo wa pili mfululizo wa ugenini, kwa idadi sawa ya mabao 5-0. Mchezo wa kwanza ukiwa dhidi ya AS Vita Club ya DR Congo.
Wekundu hao wa Msimbazi bado wako katika nafasi ya tatu kwa pointi tatu, wanayo nafasi ya kusonga mbele endapo watafanikiwa kushinda michezo yao yote iliyobakia, miwili wakicheza uwanja wao wa nyumbani na mchezo mmoja wakicheza ugenini dhidi ya JS Saoura.
0 comments:
Post a Comment