Friday, 1 February 2019

MAMA AVUA NGUO MAHAKAMANI ... ASHINDA KESI

...
Jepkosgei alikuwa akitarajia uamuzi wa kesi iliyojikokota kortini kwa muda wa miaka 10, Mama huyo aliamua kuvua nguo zote mahakamani baada ya jaji kuahirisha uamuzi wa kese hio tena kwa kudai alihitaji muda zaidi kupitia ushahidi.

Alikasirishwa na jaji na kuanza kupiga kelele kortini huku akivua nguo mbele ya umma.

Jepkosgei alishikwa na hamaki na kuvua nguo zote mbele ya Jaji Anthony Ndung’u kwa kuahirisha kesi hiyo, kwa mara nyingine.

Ndung’u alipotazamiwa kutoa uamuzi wake Alhamisi, Januari 17 kuhusu kesi hiyo iliyojikokota kortini tangu 2009, aliiahirisha kwa kudai alihitaji muda zaidi kupitia ushahidi uliowasilishwa kabla ya hatimaye kusoma uamuzi huo na hatua hiyo ikamkera sana Jepkosgei.

Jumatano, Januari 30 Katika Mahakama ya Nakuru, Jaji aliusoma uamuzi wake na kumfanya Jepkosgei kuridhika mno.

 “Kwa kufuata utaratibu naondoa amri inayomzuia Jepkemoi, msimamizi wa ardhi ya Chemerus kugawanya ardhi nambari Nakuru/Municipality Block 13/312. Msimamizi ana uhuru wa kuitumia ardhi atakavyo," Ndung'u aliamrisha.

Chanzo:Tuko
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger