Abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Bukoba mkoani Kagera kuelekea jijini Dar es salaam wamenusurika kifo huku watu wanane wakijeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao baada ya basi la Frester kupata ajali katika Kata ya Katahoka wilayani Biharamulo mkoani humo.
Gari hilo limetambulika kwa namba za usajili T375 DND ambapo mkuu wa polisi wilaya ya Biharamulo, Rashid Mududhwari amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Aidha, mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo ambaye ni diwani wa Kata ya Katahoka wilayani Biharamulo, Tulieni Abedinego Mathayo amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa jana saa 3:10 asubuhi katika kona ya kijiji cha Kasuno na kwamba kati ya majeruhi hao mwanamke mmoja amevunjika mkono.
Amesema kuwa viongozi wa wilaya wakiongozana na askari wa JWTZ Biharamulo na polisi waliwahi kuokoa abiria na kuwapelekwa Biharamulo Mjini kuwatafutia usafiri walionusurika na majeruhuhi kuwahishwa hospitali.
0 comments:
Post a Comment