Msajili
wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania Jaji Francis Mutungi ametangaza
kuvifutia usajili vyama vitatu baada ya kubainika kukiuka sheria ya
usajili wa vyama.
Vyama
hivyo ni pamoja na CHAUSTA kilichopata usajili wa kudumu tarehe 5
Novemba 2001, The African Progressive Party of Tanzania (
APPT-Maendeleo) kilichopata usajili wa kudumu terehe 4 Machi 2003 na
Chama cha Jahazi Asilia kilichopata usajili wa kudumu tarehe 17 Novemba
2004.
Jaji
Mutungi amesema kuwa mchakato wa kufuta usajili wa vyama hivyo
umetokana na zoezi la uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na
matakwa mengine ya sheria ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu
lililofanyika kuanzia tarehe 26 Juni hadi 26 Julai 2016.
Amesema
katika zoezi hilo uhakiki ulibaini kuwa vyama hivyo vimepoteza sifa za
usajili wa kudumu kwa kukiuka masharti ya sheria ya vyama vya siasa, na
kwamba kila chama kilipewa ya nia ya msajili kufuta usajili wake, lakini
vikashindwa kutoa utetezi wa kuridhisha ili visifutiwe usajili.
Kufuatia
uamuzi huo, Msajili amewataka waliokuwa wanachama wote wa vyama hivyo
kutojiuhusisha na shughuli yoyote kwa majina ya vyama hivyo, na kwamba
kufanya hivyo ni kuvunja sheria, huku akiviasa vyama vingine kuendesha
shughuli zao kwa kuzingatia sheria.
0 comments:
Post a Comment