Tamthilia ya Vaisi Vesa- sehemu ya kwanza Wivu,itazame chini ya maelezo yote hapo chini
Amani
Masuka(kushoto) na Ibrahim Songoro(kulia) wakiwa katika ofisi ya Bongo
Movie Shinyanga Jumatano,Novemba 23,2016 wakiendelea na kazi
Amani Masuka(kushoto) na Ibrahim Songoro(kulia) wakiwa katika ofisi ya Bongo Movie Shinyanga Jumatano,Novemba 23,2016
Kundi la
sanaa ya uigizaji la Swahili Arts la jijini Arusha na Bongo Movie
Shinyanga wameamua kuja upya kwa kuunganisha asasi zao na kufanya kazi
kwa pamoja ili kuhakikisha wanaiwakilisha vyema Shinyanga na
kuitambulisha tasnia ya filamu mkoa wa Shinyanga.
Wakizungumza
na Malunde1 blog,wamesema sasa wameamua kuja kwa ujio mpya ambao
utakuwa bandika bandua kwa kazi zenye ubora na mafunzo na wameanza kwa
tamthiliya ya Vaisa Vesa.
Hatua
hiyo imekuja baada ya mwongozaji wa filamu nchini Amani Masuka
anayeongoza kundi la sanaa ya uigizaji la Swahili Arts la jijini Arusha
na mmliki wa Eden Media Creation,kumaliza tofauti zilizojitokeza
mwanzoni mwa mwaka 2015 na Bongo Movie Shinyanga inayosimamiwa na
Ibrahim Songoro ambaye pia anamiliki Songoro Media Production.
Pamoja na
mikakati kibao waliyonayo itakayoanza mwezi Desemba 05 mwaka
huu,magwiji hao wa sanaa ya uigizaji na uongozaji wa filamu wameahidi
kuja na mkakati utakaotengeneza wasanii wapya na kujenga misingi imara
ya kiwanda cha filamu mkoa wa Shinyanga.
Tayari
wameanza na tamthilia fupi inayojulikana kwa jina la 'Vaisi Vesa'
itakayokuwa inarushwa kwa njia ya mitandao ya kijamii kama vile
youtube,instagram,whatsapp n.k.
Wahusika wakuu katika tamthilia hiyo ni Ibrahim Songoro na Miss Grace,mwongozaji ni Masuka A.J na mpiga picha ni David Skerah.
Mwandishi
na mwongozaji wa tamthilia ya Vaisi Vesa,Amani Masuka amesema filamu
hiyo imejaa visa mbalimbali vinavyotokea katika maisha ya binadamu
vinavyotokana na watu wawili kupishana kauli.
“Tamthilia
ya Vaisi Vesa itakuwa inatoa visa vifupi ambavyo wahusika huwa
wanatofautiana kauli ‘kauli tata’,itakuwa inahusisha watu
wawili”,anaeleza Masuka.
Amesema
sehemu ya kwanza ya tamthiliya hii inaitwa “Wivu”,ambapo utata umeibuka
kutokana na kauli ya “Ugonjwa usiokuwa na tiba”,ambapo mhusika mkuu
Ibrahim Songoro anatafsiri ugonjwa usio na tiba kuwa ni Ukimwi ilhali
binti aliyekuwa anamshawishi awe mpenzi wake akimaanisha ugonjwa usio na
tiba kuwa ni wivu.
“Hapo
tunaona unafiki wa Songoro anayewakilisha wanaume walaghai akibadilika
ghafla na kumshtumu binti huyo kuwa ni muuaji aliyekusudia kumwambukiza
virusi vya Ukimwi”,anaeleza Masuka.
“Binti
anajitahidi kumwelewesha Songoro kuwa alimaanisha wivu,ndipo Songoro
anarudi kinafiki na kuanza kujichekesha,hapa tunapata ujumbe kuwa siyo
kila neno unaloambiwa unatakiwa kuliamini(wanawake),lakini pia kabla ya
kuchukua maamuzi unapaswa kufikiria sana kabla ya kutoa uamuzi ulio
sahihi (wanaume)”,ameongeza Masuka.
Akizungumzia
tamthilia hiyo, mwenyekiti wa Bongo Movie Shinyanga Ibrahim Songoro
“Songoro Gaddafi” amesema tamthiliya ya Vaisi Vesa imelenga
kuielimisha,kuiburudisha na kuikosoa jamii katika masuala mbalimbali.
Kwa
taarifa zaidi kuhusu tamthilia ya Vaisi Vesa na mambo mengine ya sanaa
ya uigizaji wasiliana na Ibrahim Songoro kwa simu namba 0767831036 na
Amani Masuka simu namba 0767856192.
Tumia dakika zako chache kutazama Tamthilia ya Vaisi Vesa hapa chini katika sehemu yake ya kwanza inayoitwa “Wivu”.
0 comments:
Post a Comment