Taarifa ya Sherehe za Mahafali ya 32 ya Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo.
Uongozi wa
Chuo Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo unayo furaha kuwafahamisha wahitimu
wote, wanajumuiya wote wa Chuo na umma kwa ujumla, kuwa sherehe ya Mahafali ya 32 ya Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo, itafanyika Ijumaa tarehe 25 Novemba, 2016 katika Kampasi ya Solomon Mahlangu “Nelson Mandela Freedom Square” Mazimbu, kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Sherehe hiyo itatanguliwa na sherehe ya utoaji zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri sana katika masomo yao “Prize awarding Ceremony” hapo alhamisi tarehe 24 Novemba, 2016 katika ukumbi wa mikutano wa baraza la Chuo yaani “Council Chamber” uliopo kampasi kuu, kuanzia saa 2:30 hadi saa 4:30 asubuhi.
Aidha, mkutano wa majalisi ya wanataaluma wa SUA yaani “Annual general meeting of SUA convocation” utafanyika siku hiyo ya Alhamisi tarehe 24 Novemba, 2016 “Multipurpose hall” kampasi kuu, kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi saa 7:00 mchana.
Wahitimu ˝Graduands˝ wanakumbushwa kushiriki katika mazoezi ˝Rehearsal˝ yatakayofanyika 25 Novemba, 2016 kuanzia saa 2.00 hadi saa 3.00 asubuhi, “Nelson Mandela Freedom Square”, kampasi ya solomon mahlangu, mazimbu.
Wote Mnakaribishwa.
Imetolewa Na:
Kitengo Cha Mawasiliano Na Masoko, SUA
Kitengo Cha Mawasiliano Na Masoko, SUA
>>KUONA MAJINA YA WAHITIMU BONYEZA HAPA<<
0 comments:
Post a Comment